

Lugha Nyingine
Kampuni ya “midoli pendwa ya bata” yakita mizizi Qianhai, Shenzhen, China ikisambaza “rangi ya dhahabu” kwa mashabiki milioni 200 duniani
Mdoli wa B. Duck ukiwa kwenye ofisi ya Kampuni ya B.Duck Qianhai, Shenzhen, China (Picha/People's Daily Online)
Kampuni ya B.Duck, kampuni kubwa na maarufu ya midoli pendwa duniani iliyoanzishwa mjini Hong Kong Mwaka 2025 imekuwa ikikua kwa kasi na sasa imekita mizizi yake katika eneo la Qianhai, Shenzhen, China ikiunga mkono maendeleo bora ya kiwango cha juu ya Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao huku ikisambaza bidhaa zake bora duniani kote.
Jina hilo la B.Duck, ambalo kwa tafsiri ya moja kwa moja ya Kiswahili ni B. Bata na kwa Kichina ikivuma kwa jina la "Bata Mdogo wa Njano" linahamasishwa zaidi na miundo yake ya kuvutia ya bidhaa zenye umbo la bata, ikitawaliwa zaidi na rangi ya njano, rangi ambayo pia hurejelewa kama rangi ya dhahabu.
Mchanganyo huo wa umbo la bata na rangi hiyo ya njano, umeleta bidhaa mbalimbali bora ambazo zimekuwa zikivutia mamilioni ya mashabiki katika nchi na maeneo mbalimbali, zikisambaza rangi ya dhahabu na bata huyo kote duniani.
Kwa mujibu wa nyaraka kutoka kampuni hiyo, bidhaa nyingi za kampuni hiyo, kama vile za midoli mbalimbali pendwa, mavazi, mabegi, baiskeli, mapambo, mifuko, vitu vya kuchezea watoto na nyingine nyingi, si tu zimekuwa zikiteka masoko na kuvutia wimbi kubwa la ununuzi bali pia ni maarufu sana miongoni mwa vijana wa vizazi vya milenia na Z wanaopendelea bidhaa zinazovuma na za mitindo ya kisasa.
Mathalani, inaelezwa kuwa kampuni hiyo ina mashabiki zaidi milioni 23 duniani kote. Imetoa leseni zaidi ya 500 kwa kampuni kuzalisha bidhaa kwa chapa yake katika maeneo mengi ya China, Asia Kusini Mashariki, na Amerika Kusini, huku bidhaa na biashara zaidi ya 25,000 zikizalishwa chini ya leseni yake.
Aidha, imeshafanya shughuli zaidi ya 100 zenye maudhui kuhusu bidhaa zake kwenye maduka makubwa, zikiwa na wastani wa mahudhurio ya watu zaidi ya milioni 1.2 kwa kila shughuli, yakifikia jumla ya watu milioni 240.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma