

Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa UM asema mapendekezo ya dunia yaliyotolewa na China yanaendana na katiba ya UM
(Xinhua/Xie E)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema jana tarehe 16 kuwa mapendekezo ya dunia yaliyotolewa na China yanaendana kikamilifu na Katiba ya Umoja wa Mataifa.
Akiongea na wanahabari Bw. Guterres amesema mapendekezo hayo yaliyotolewa na China yameheshimu kikamilifu mahusiano ya pande nyingi, na yameunga mkono Umoja wa Mataifa kuwa kiini cha mfumo wa pande nyingi na pia kulenga kuhimiza ushirikiano wa kimataifa na kutatua migogoro kwa njia ya amani.
Pia ameongeza kuwa wiki ijayo shughuli za Wiki ya Ngazi ya Juu ya Baraza Kuu la 80 la Umoja wa Mataifa zitafanyika, ambapo viongozi na wakuu wa nchi takriban 150 watashiriki kwenye shughuli hizo, na atatumia fursa hiyo kuwahimiza viongozi hao kuimarisha mawasiliano, kufanya mazungumzo na kutafuta suluhisho kwa masuala mbalimbali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma