

Lugha Nyingine
Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa yathibitisha Israel ilifanya mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza
(CRI Online) Septemba 17, 2025
Tume Huru ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa juu ya ardhi za Palestina zinazokaliwa na Israel na masuala ya Israel, jana imetoa ripoti ikisema, Israel imefanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza.
Tume hiyo imezitaka Israel na nchi zingine zote zitekeleze majukumu yao kwa sheria za kimataifa, kukomesha matukio hayo ya mauaji ya kimbari, na kuwaadhibu wahusika.
Ripoti hiyo imesema kuwa dhamira ya vitendo hivi vya mauaji ya kimbari ni kuangamiza kikamilifu au baadhi ya Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma