Zambia yapongeza uamuzi wa IMF wa kuongeza muda wa mpango wa mkopo

(CRI Online) Septemba 17, 2025

Serikali ya Zambia imepongeza uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wa kuridhia ombi la nchi hiyo la kuongeza makubaliano ya Mpango wa Mikopo ya Muda Mrefu (ECF).

Jumatatu wiki hii, Bodi hiyo iliikubalia Zambia nyongeza ya miezi mitatu ya mpango wa ECF, ikihamisha tarehe ya mwisho kuwa Januari 30, 2026 hatua inayotarajia kutoa muda zaidi wa kukamilisha tathmini ya 6 ya mpango huo na kuandaa njia ya ushirikiano wa baadaye.

Waziri wa Fedha na Mipango ya Kitaifa wa nchini humo, Situmbeko Musokotwane amethibitisha uamuzi huo, akisema unaakisi imani ya IMF kwa Zambia katika juhudi za mageuzi nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha