Malawi yapiga kura katika uchaguzi mkuu

(CRI Online) Septemba 17, 2025

(Xinhua/Peng Lijun)

(Xinhua/Peng Lijun)

Zoezi la kupiga kura katika uchaguzi mkuu nchini Malawi lilianza rasmi saa 12 asubuhi na kukamilika saa 10 jioni kwa saa za huko hapo jana, na zaidi ya wapiga kura milioni 7.2 waliojiandikisha watachagua rais, wajumbe wa Bunge la Kitaifa, na madiwani wa maeneo.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa rais wa sasa ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha Malawi Congress Party Lazarus Chakwera, na Rais wa zamani ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Democratic Progressive Party Peter Mutharika wanaongoza.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi, duru ya kwanza ya matokeo ya uchaguzi wa urais itatangazwa kabla ya tarehe 24 mwezi huu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha