

Lugha Nyingine
Xi Jinping: Maadhimisho ya siku ya ushindi ya China yaongeza Imani ya kuhimiza ustawishaji wa taifa
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, akikutana na wajumbe wa sekta mbalimbali walioshiriki kwenye maandalizi ya maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti kwenye Jumba kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Septemba 17, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)
Maadhimisho ya siku ya ushindi ya China yameimarisha imani ya nchi ya kujenga nchi yenye nguvu zaidi na kuhimiza ustawishaji wa taifa kwa pande zote, amesema rais Xi Jinping.
Rais Xi alisema hayo katika hotuba yake ya hivi karibuni, baada ya kusikiliza ripoti ya kufanya majumuisho kuhusu shughuli za kuadhimisha miaka 80 ya ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti.
Hotuba ya Xi, ambayo ilitolewa kwenye mkutano wa wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, iliwasilishwa Jumatano katika mkutano wa kufanya majumuisho kuhusu shughuli za kuadhimisha.
Kwenye Jumba kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, Xi alikutana na wajumbe wa sekta mbalimbali walioshiriki kwenye maandalizi ya maadhimisho, akipongeza mchango uliotolewa nao na mafanikio yaliyopatikana, na kuwatia moyo kujipatia mafanikio mapya.
Katika hotuba yake, Xi alisema kuwa maadhimisho yalichangamsha na kutia hamasa, na yameenzi moyo mtukufu uliotokana na Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan.
“Shughuli hizo zilionesha uwajibikaji wa China katika kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja,” Xi alisema.
Xi alisisitiza mahitaji ya kuendelea kutumia shughuli za maadhimisho kuwa mafunzo ya uzalendo, na kubadilisha imani, fahari na uhai vilivyochochewa kuwa nguvu kubwa ya kusukuma mbele mageuzi, maendeleo na utulivu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma