

Lugha Nyingine
Ripoti ya WTO yasema AI yatarajiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara duniani
Shirika la Biashara Duniani (WTO) jana lilitoa Ripoti ya Biashara Duniani 2025, likitabiri kwamba, kwa sera zinazofaa, utumiaji wa akili bandia (AI) unatarajiwa kuongeza ukuaji wa biashara ya kimataifa kwa karibu 40% ifikapo mwaka 2040.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa WTO Bi. Ngozi Okonjo-Iweala alibainisha kuwa, AI ina uwezo mkubwa wa kupunguza gharama za biashara na kuongeza tija. Hata hivyo, uwezo wa makundi mbalimbali ya kiuchumi wa kumiliki teknolojia za AI na uwezo wa kushiriki katika biashara ya kidijitali bado unakabiliwa na tofauti kubwa.
Ripoti hiyo pia imesema, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, hasa katika eneo la AI na biashara ya kidijitali, kutawezesha makundi mbalimbali ya kiuchumi kujishughulisha katika maendeleo ya AI, na kwamba WTO inaweza kuchangia zaidi katika kuhakikisha ukuaji wa biashara shirikishi kupitia teknolojia ya AI.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma