

Lugha Nyingine
Treni ya teknolojia za kisasa yenye viwango vya China ya kutoa huduma kati ya miji yaoneshwa kwa mara ya kwanza Qingdao, China (2)
![]() |
Watu wakitembelea treni ya teknolojia za kisasa yenye viwango vya China ya kutoa huduma kati ya miji, Septemba 18, 2025. (Xinhua/Li Ziheng) |
Treni ya teknolojia za kisasa yenye viwango vya China ya kutoa huduma kati ya miji, ikiwa na hakimiliki za uvumbuzi zinazomilikiwa kikamilifu na China kwa kujitegemea, imeoneshwa kwa mara ya kwanza mjini Qingdao, China, Tarehe 18, Septemba.
Treni hiyo itatumika kwenye Reli ya Huduma za Usafiri wa Haraka kati ya Mji wa Beijing na Mji wa Xiong’an.
Treni hiyo iliyoundwa katika mfumo wa viwango vya China, na ikijumuisha teknolojia muhimu zilizovumbuliwa na China kwa kujitegemea, ina uwezo wa kujiendesha kiotomatiki kwa Daraja la GOA4 kwa kasi ya kilomita 200 kwa saa.
Aidha, inajumuisha teknolojia muhimu za kivumbuzi zaidi ya kumi, ikifikia uboreshaji kamili wa kina katika AI, usafiri salama na tulivu, uhifadhi nishati, na uendeshaji kwa gharama nafuu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma