Lugha Nyingine
Uganda yathibitisha UAE kuweka vizuizi vipya vya viza
(CRI Online) Septemba 19, 2025
Waziri wa Nchi anayeshughulika Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Uganda, Oryem Henry Okello amesema Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umeongeza matakwa ya viza kwa raia wa Uganda kukutokana na wasiwasi unaoongezeka juu ya unyanyasaji wa wahamiaji na uhalifu unaofanywa na baadhi ya wasafiri.
Amesema UAE imeamua kusitisha utoaji wa visa ya muda mrefu kwa baadhi ya raia wa Uganda, lakini akasisitiza kuwa hatua hiyo hailingani na marufuku kamili ya kusafiri.
UAE imetangaza kupiga marufuku viza kwa mwaka 2026, na kuwazuia raia wa nchi kadhaa za Afrika na Ulaya, ikiwemo Uganda, kuomba viza ya utalii na kazi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



