Lugha Nyingine
Watu 31 wafariki katika mlipuko wa karibuni wa Ebola nchini DRC
(CRI Online) Septemba 19, 2025
Ofisa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Patrick Otim amesema, watu 31 wamefariki katika mlipuko wa hivi karibuni wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari wa mtandaoni, Otim amesema kesi 48 zimeripotiwa katika mkoa wa Kasai katikati ya DRC, zikiwemo 38 zilizothibitishwa kuwa na maambukizi. Amesema wagonjwa 31 wamefariki, huku wengine 15 wakiendelea na matibabu katika kituo cha Ebola huko Bulape, ambako mlipuko huo ulitokea, na wagonjwa wawili wameruhusiwa kutoka hospitali.
Otim amesema, kampeni ya chanjo imeanza, na karibu dozi 760 zimepelekwa Bulape, ambapo zaidi ya wafanyakazi wa afya 500 na watu waliowasiliana kwa karibu na wagonjwa wamepata chanjo hizo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



