Lugha Nyingine
Rais wa Zimbabwe ahimiza ushirikiano imara zaidi na China
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametoa wito kwa chama tawala nchini humo ZANU-PF, serikali, na sekta binafsi kuboresha ushirikiano na China kufuatia kupanda ngazi ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Akihutubia katika kikao cha 387 cha Kamati Kuu ya Chama hicho kilichofanyika Harare, mji mkuu wa nchi hiyo, rais Mnangagwa amesema ziara yake ya hivi karibuni nchini China imeonyesha nia thabiti ya Zimbabwe kuimarisha uhusiano na kuboresha ushirikiano na China kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa Zimbabwe.
Mapema mwezi huu, rais Mnangagwa alihudhuria maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi wa China dhidi ya uvamizi wa Japan na ushindi wa dunia dhidi ya vita ya ufashisti, ambapo pande hizo mbili za China na Zimbabwe zilikubaliana kuongeza ngazi ya uhusiano wao kuwa wa pande zote wenye mustakabali wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



