Kampuni ya China yatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko nchini Sudan Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 19, 2025

Kampuni ya China jana Alhamis imetoa vifaa vya msaada kwa maelfu ya watu waliokosa makazi kutokana na mafuriko yaliyotokea katika Jimbo la Unity kaskazini mwa Sudan Kusini.

Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano ya umma katika Shirika la Kitaifa la Petroli la China (CNPC) Ren Yongshen amesema, msaada huo ni pamoja na mahema, mablanketi, mikeka, vyandarua, na dawa za malaria. Amesema wanatarajia kuwa msaada huo utawapa nafuu wahanga wa mafuriko hayo, na kuongeza kuwa, kwa miaka kadhaa, kampuni hiyo imechangia zaidi ya dola za kimarekani milioni 6 kwa miradi ya hisani nchini Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, karibu watu 273,000 wameathiriwa na mafuriko katika kaunti 12 katika majimbo ya Jonglei, Unity, Upper Nile, na Ikweta ya Kati.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha