

Lugha Nyingine
Rais Xi ahudhuria mkusanyiko mkubwa wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihudhuria mkusanyiko mkubwa wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang huko Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo kaskazini magharibi mwa China, Septemba 25, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
URUMQI - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amehudhuria mkusanyiko mkubwa katika kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang jana Alhamisi huko Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo kaskazini-magharibi mwa China ambapo akiwa pamoja na makada na watu wa makabila na sekta mbalimbali mkoani Xinjiang kuhudhuria kwenye mkusanyiko huo.
Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China (CPPCC) na mkuu wa ujumbe wa kamati kuu ya Chama na serikali kuu alihudhuria pia kwenye mkusanyiko huo. Cai Qi, mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC pia alikuwepo kwenye mkusanyiko huo, Wang na Cai wote ni wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati kuu ya Chama.
Mkusanyiko huo ulianza majira ya saa 4:30 asubuhi. Washiriki wote walisimama na kuimba wimbo wa taifa.
Ujumbe wa pongezi kutoka Kamati Kuu ya CPC, Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Baraza la Serikali la China, Kamati ya Kitaifa ya CPPCC, na Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ulisomwa kwenye mkusanyiko huo.
Katika hotuba yake, Wang amesema katika miaka 70 iliyopita, watu wa makabila mbalimbali mkoani Xinjiang wamepata mafanikio makubwa katika mapinduzi ya kijamaa, maendeleo ya mambo, mageuzi na ufunguaji mlango, chini ya uongozi wa CPC.
"Xinjiang, pamoja na sehemu mbalimbali nchini China, zimeshinda vita dhidi ya umaskini na kufikia malengo ya ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote," amesema Wang, akisema kuwa mshikamano wa makabila mkoani Xinjiang umeimarishwa zaidi, na watu wameongeza uelewa juu ya jumuiya ya pamoja ya taifa la China.
Wang amesema mafanikio yaliyopatikana katika mkoa huo unaojiendesha katika miongo saba iliyopita yameonesha nguvu bora za uongozi wa Chama na mfumo wa kijamaa, vilevile nguvu kubwa ya kushughulikia masuala ya makabila kwa usahihi na kwa njia pekee yenye umaalumu wa China.
Ametoa wito wa kufanya juhudi za kuijenga Xinjiang ya mambo ya kisasa ya kijamaa iliyo ya mshikamano, maafikiano, ustawi, utajiri, maendeleo ya utamaduni na mazingira mazuri ya kiikolojia, ambapo watu wanaishi na kufanya kazi kwa furaha katika hali ya utulivu.
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihudhuria mkusanyiko mkubwa wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang huko Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo kaskazini magharibi mwa China, Septemba 25, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihudhuria mkusanyiko mkubwa katika kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang huko Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo kaskazini magharibi mwa China, Septemba 25, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihudhuria mkusanyiko mkubwa wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang huko Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo kaskazini magharibi mwa China, Septemba 25, 2025. (Xinhua/Shen Hong)
Wang Huning, mjumbe wa udumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China na mkuu wa ujumbe wa mamlaka kuu, akitoa hotuba kwenye mkusanyiko mkubwa wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang huko Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo kaskazini magharibi mwa China, Septemba 25, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma