China na Marekani zinahitaji kutafuta njia sahihi ya kupatana katika zama mpya - Waziri Mkuu wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwa katika picha ya pamoja na washiriki kabla ya mkutano wake na mashirika rafiki nchini Marekani pembezoni mwa mjadala wa jumla wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mjini New York, Marekani, Septemba 25, 2025. (Xinhua/Wang Ye)

NEW YORK - Waziri Mkuu wa China Li Qiang kwenye mkutano na mashirika rafiki nchini Marekani, wakiwemo wawakilishi kutoka Baraza la Biashara la Marekani na China, Kamati ya Kitaifa ya Uhusiano kati ya Marekani na China, Shirikisho la Wafanyabiashara wa Marekani na Baraza la Uhusiano wa Kigeni, vilevile wasomi na viongozi wa biashara, amesema kwamba kwa kutazama siku za baadaye, China na Marekani zinahitaji kutafuta njia mpya ya kupatana katika zama mpya.

"Uhusiano kati ya China na Marekani ni uhusiano muhimu zaidi wa pande mbili duniani, na nchi hizo mbili zinaweza na zinapaswa kuwa washirika na marafiki," Li amesema kwenye mkutano huo uliofanyika jana Alhamisi pembezoni mwa mjadala wa jumla wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.

"Tukitazama nyuma katika historia, mawasiliano ya kirafiki kati ya China na Marekani yamekuwa ya kawaida na mwelekeo wa jumla," Li amesema.

Amesema, kama Rais Xi Jinping wa China alivyosema, upana wa Bahari ya Pasifiki ni mkubwa kutosha kuzikumbatia China na Marekani, vilevile nchi nyinginezo.

Li amesema, zikiwa nchi mbili kubwa duniani China na Marekani zinapaswa kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani, kutafuta ushirikiano wa kunufaishana, na kupata ustawi wa pamoja kupitia kufanikishana.

Amesema, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara ni sehemu muhimu ya uhusiano wa pande mbili.

Li ameongeza kuwa, kwa kuzingatia miundo yao tofauti ya soko na miundo ya kiviwanda inayokamilishana sana, vilevile nafasi yao kubwa katika minyororo ya viwanda duniani, ushirikiano wa karibu wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani utazinufaisha nchi hizo mbili na dunia kwa ujumla.

Amesema China ina imani na uwezo wa kudumisha maendeleo tulivu na mazuri ya uchumi, na kuunda fursa zaidi kwa kampuni kutoka duniani kote, zikiwemo kampuni za Marekani.

Jumuiya hiyo ya wafanyabiashara wa Marekani imeelezea matumaini yake kuhusu matarajio ya maendeleo ya uchumi wa China na nia yake ya kuendelea kupanua uwekezaji nchini China ili kutekeleza jukumu la kuwa daraja la kuhimiza ushirikiano wa pande mbili na kuongeza maelewano. 

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na mashirika rafiki nchini Marekani pembezoni mwa mjadala wa jumla wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mjini New York, Marekani, Septemba 25, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha