Tamasha la Kimataifa la Sarakasi lafunguliwa katika "maskani ya sarakasi" ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 29, 2025
Tamasha la Kimataifa la Sarakasi lafunguliwa katika
Wanasarakasi wakifanya maonesho kwenye hafla ya ufunguzi wa Tamasha la 20 la Kimataifa la Sarakasi la Wuqiao China katika Wilaya ya Wuqiao, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China, Septemba 28, 2025.(Xinhua/Mu Yu)

SHIJIAZHUANG - Tamasha la 20 la Kimataifa la Sarakasi la Wuqiao China limefunguliwa rasmi jana Jumapili katika Wilaya ya Wuqiao, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China, ikiwa ni mara ya kwanza kwa shughuli hiyo kufanyika katika "maskani ya sarakasi" maarufu ya China.

Tamasha hilo linashirikisha wasanii 28 kutoka nchi na maeneo 19, wakiwania tuzo tatu za Simba wa Dhahabu, tano za Simba wa Fedha na saba za Simba wa Shaba. Hafla ya kufunga imepangwa kufanyika Oktoba 3, huku shughuli husika za tamasha hilo zikiendelea hadi Oktoba 8, siku ya mwisho ya siku nane zijazo za Sikukuu ya Taifa na Sikukuu ya Mbalamwezi Katikati mwa Majira ya Mpukutiko.

Maonyesho ya programu maalum 12 za sarakasi za kiwango cha juu za China zilizofadhiliwa katika miaka ya hivi karibuni na Mfuko wa Sanaa wa Kitaifa wa China yamefanyika jana Jumapili, yakionyesha mafanikio katika sanaa ya sarakasi ya China. Shughuli nyingine zilijumuisha maonyesho ya sarakasi na maonyesho ya urithi wa utamaduni usioshikika wa Mfereji Mkuu wa China.

Likiwa lilianzishwa mwaka 1987 na kufanyika kila baada ya miaka miwili, Tamasha hilo ni shughuli kubwa na yenye ushawishi mkubwa zaidi katika sanaa ya sarakasi nchini China, vile vile ni moja ya mashindano ya kimataifa yenye maonesho mengi ya kisanaa na Shughuli za Utamaduni yanayofanyika nchini China.

Tamasha hilo linachukuliwa kuwa moja ya mashindano matatu makubwa ya sarakasi duniani, sambamba na Tamasha la Kimataifa la Sarakasi la Monte-Carlo mjini Monaco na Tamasha la Sarakasi Duniani la Kesho mjini Paris.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha