Ujenzi wa Kituo Kipya cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baiyun wa Guangzhou wakamilika kwa sehemu kubwa kusini mwa China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 30, 2025
Ujenzi wa Kituo Kipya cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baiyun wa Guangzhou wakamilika kwa sehemu kubwa kusini mwa China
Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi Agosti 24, 2025 ikionyesha mwonekano wa Majengo ya T3 (kushoto), T1 na T2 (kulia) ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baiyun wa Guangzhou katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China. (Xinhua/Liu Dawei)

Ujenzi wa kituo kipya cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baiyun wa Guangzhou katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China umekamilika kimsingi hivi karibuni. Jengo hilo linatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwaka 2025.

Baada ya kukamilika na kuanza kutumika rasmi, Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 120 kwa mwaka na uwezo wa jumla wa kushughulikia mizigo na vifurushi vinavyopita vya uzito wa tani milioni 3.8.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha