Lugha Nyingine
Wafanyakazi Wachina wasaidia kujenga alama mpya ya Misri (7)
![]() |
| Picha iliyopigwa Oktoba 5, 2025 ikionyesha mwonekano wa Eneo la Kati la Biashara (CBD) katika mji mkuu mpya wa utawala nje kidogo ya Cairo, Misri. (Picha na Li Binghong/Xinhua) |
CAIRO - Wakati familia nyingi za Wachina zilipokuwa zikisherehekea sikukuu ya Mbalamwezi, sikukuu ya jadi ya katikati mwa majira ya mpukutiko, kundi la wajenzi Wachina walikuwa wakifanya kazi kwenye Eneo la Kati la Biashara (CBD) katika mji mkuu mpya wa utawala wa Misri nje kidogo ya Cairo.
Shamrashamra za sherehe zilikuwa zimeshika kasi nyumbani, lakini wafanyakazi hao Wachina walichagua kubaki kwenye eneo la ujenzi wa jengo lenye ghorofa 20 la CBD, kuratibu kazi za kwenye eneo la ujenzi, kumaliza mambo ya ndani, na kukamilisha maghorofa hayo marefu ambayo punde yatakuwa alama ya baadaye ya maghorofa marefu ya Misri tayari kwa makabidhiano ya mwisho.
Hu Yingdong, msimamizi wa Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la Serikali ya China (CSCEC), amesema kazi yake inahusisha kuratibu mafunzo ya usalama wa kila siku, kugawa majukumu ya kwenye eneo la ujenzi, na kusaidia wasimamizi kwa ukaguzi na uidhinishaji.
"Kazini, wafanyakazi Wachina wanachangia uzoefu wa kiufundi na viwango na wenzao wa Misri ili kuboresha sifa bora na ufanisi. Katika maisha, tumejenga urafiki mkubwa, tukisaidiana kama ndugu," Hu ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.
Mradi huo wa CBD una majengo 10 ya ofisi, maghorofa matano ya makazi, hoteli nne kubwa, na Ghorofa la Kipekee lenye urefu wa mita 385.8, jengo refu zaidi barani Afrika.
Kwa wafanyakazi hao, mradi unabeba urafiki kati ya China na Misri na unaonyesha dhamira ya wajenzi katika weledi kwenye teknolojia, ubora na ulinzi wa mazingira.
Kwa mfano, kutumiwa kwa teknolojia ya chute ya Kichina kumehakikisha mchakato salama na fanisi wa kumwaga zege; Maji machafu yamesafishwa kuwa safi na kutumika tena; Paneli za jua zilizofungwa kwenye paa zimewezesha nishati mbadala kutosheleza sehemu ya mahitaji ya nishati.
Mradi huo umezalisha makumi kwa maelfu ya nafasi za ajira kwa wenyeji, kuongeza uwezo wa wafanyakazi wa Misri, na kukuza uhusiano mkubwa wa mkufunzi-mfunzwa kati ya wafanyakazi wa China na Misri.
"Kilichonigusa zaidi, ni kwamba kila mara wakati mkataba wa mfanyakazi Mchina unapomalizika na akitakiwa kurejea nyumbani, wafunzwa wake kadhaa wa Misri hukimbia kutoka eneo la ujenzi ili kumuaga kwa mguso kutoka moyoni." Hu amesema.
CBD ni mradi wa kihistoria chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lililotolewa na China (BRI), ambao unafuata maendeleo ya pamoja miongoni mwa nchi zinazoshiriki.
Ukiwa ulizinduliwa mwaka 2018, mradi huo umekabiliana na mfululizo wa changamoto kwa miaka mingi, kutoka janga la COVID-19 na kuvurugwa kwa usafirishaji wa meli kimataifa hadi kushuka na kupanda kwa sarafu ya Misri na kupanda kwa gharama za nyenzo. Licha ya vizuizi hivi, mradi umeendelea kusonga mbele kwa kasi, kutokana na juhudi zinazoendelea za timu zote za China na Misri kufanya kazi bega kwa bega.
Kwa Huang Changbiao, naibu meneja mkuu wa CSCEC Tawi la Misri, mradi huo unasimama kama "mfano wa mfungamano wa kina kati ya BRI ya China na Dira ya Misri ya 2030."
"Unawakilisha mfano mzuri wa ujenzi wa China kwenye Ukanda Mmoja, Njia Moja," amesema, akiongeza kuwa wafanyakazi wapatao 5,000 wa China na Misri wataendelea kujitahidi kukamilisha mrada huo alama mpya ya Misri haraka iwezekanavyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




