

Lugha Nyingine
Wanandoa 263,000 wa China wanufaika na utaratibu uliorahisishwa wa usajili wa ndoa (7)
![]() |
Lu Zhiyuan, waziri wa mambo ya kiraia wa China, na Li Changguan, Hu Haifeng, na Liu Zhenguo, wote manaibu mawaziri wa mambo ya kiraia, wakihudhuria mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China (SCIO) kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika mambo ya raia katika kipindi cha Mpango wa 14 wa Miaka Mitano (2021-2025) mjini Beijing, Oktoba 10, 2025. (Xinhua/Li Xin) |
BEIJING – Wizara ya Mambo ya Kiraia ya China imesema jana kuwa, wanandoa zaidi ya 263,000 wa China wamenufaika na utaratibu uliorahisishwa wa usajili wa ndoa bila kujali sehemu wanakotoka tangu ulipoanza kutekelezwa Mei 10 mwaka huu, ambapo utaratibu huo mpya unaruhusu wanandoa kusajili ndoa zao katika ofisi yoyote rasmi ya usajili nchini kote, bila kujali hao ni wakazi wa sehemu gani.
Aidha, wanandoa sasa wanahitaji tu kuonesha vitambulisho vyao kwa kusajiliwa, ikiondoa hitaji la muda mrefu la kuonesha vijitabu vya sehemu za usajili wa nyumbani kwao.
Waziri wa mambo ya kiraia Lu Zhiyuan ameuambia mkutano na waandishi wa habari kwamba mabadiliko ya mila na desturi za ndoa yanaendelea kutokea kwa kina nchini China, ambapo mwelekeo wa maendeleo ya hali nzuri zaidi ya mila na desturi za ndoa ukionekana kwa haraka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma