Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake waanza leo mjini Beijing, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 13, 2025
Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake waanza leo mjini Beijing, China
Mabango ya mtaani kwa ajili ya Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake yakionekana mjini Beijing, China, Oktoba 11, 2025. (Xinhua/Ju Huanzong)

BEIJING - Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake unafanyika Beijing, mji mkuu wa China, kuanzia Tarehe 13 hadi 14 Oktoba.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya China wiki iliyopita ilieleza kuwa, mkutano huo unaoandaliwa kwa pamoja na China na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women), utawakutanisha wakuu wa nchi, viongozi wa serikali, viongozi wa mabunge, manaibu mawaziri wakuu, maofisa wa wizara, viongozi wa mashirika ya kimataifa na watu marafiki kutoka mabara mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha