

Lugha Nyingine
Walinzi wa Pwani ya China wafukuza meli za Ufilipino zilizoingia kinyume cha sheria kwenye maji karibu na Kisiwa cha Tiexian
![]() |
Chombo cha majini cha Ufilipino 3003 kikingia kinyume cha sheria ndani ya maji karibu na Kisiwa cha Tiexian katika Bahari ya Kusini ya China, Oktoba 12, 2025. (CCG/kupitia Xinhua) |
BEIJING - Askari Polisi wa Ulinzi wa Bahari wa China wamezifukuza meli za Ufilipino zilizoingia kinyume cha sheria ndani ya maji karibu na Kisiwa cha Tiexian Jiao katika Bahari ya Kusini ya China jana Jumapili, msemaji wa askari polisi wa bahari Liu Dejun amesema.
Liu amesema, meli za shughuli za kiserikali za Ufilipino za namba 3002 na 3003 ziliingia kinyume cha sheria kwenye maji karibu na Kisiwa cha Tiexian Jiao cha Visiwa vya Nansha vya China bila kibali cha serikali ya China.
Liu ameongeza kuwa, saa 3:19 asubuhi, meli ya Ufilipino No.3003 ilipuuza onyo lililotolewa mara kadhaa na upande wa China ikikaribia kwa hatari meli ya CCG 21559, ambayo ilikuwa ikifanya kazi ya kawaida ya kulinda haki na kutekeleza sheria, na kusababisha hali ya kugongana.
"Wajibu kamili uko kwa upande wa Ufilipino," Liu amesisitiza.
Amesema kuwa, CCG ilichukua hatua za udhibiti kwa mujibu wa sheria dhidi ya meli za Ufilipino na kuzifukuza kithabiti. Amesema hatua hizo zimefanywa kwa weledi, kufuata kanuni, kwa busara na kisheria.
Msemaji huyo amesisitiza kuwa China ina mamlaka isiyopingika juu ya Visiwa vya Nansha, kikiwemo kisiwa cha Tiexian na maeneo ya bahari ya karibu navyo, na vitendo vya upande wa Ufilipino vimevamia vibaya mamlaka ya ardhi ya China, kukiuka Azimio la Vitendo vya Pande husika katika Bahari ya Kusini ya China, na kuharibu amani na utulivu katika Bahari ya Kusini.
"Tunaionya vikali Ufilipino kuacha mara moja ukiukaji na vitendo vya uchokozi. Askari Polisi wa bahari watafanya shughuli za kulinda haki na kutekeleza sheria kama kawaida katika eneo la bahari la mamlaka ya China kwa mujibu wa sheria," Liu amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma