Wageni waingia Mkoa wa Hainan wa China chini ya sera nzuri ya msamaha wa visa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 16, 2025
Wageni waingia Mkoa wa Hainan wa China chini ya sera nzuri ya msamaha wa visa
Abiria wanaoingia China wakipitia taratibu za ukaguzi wa mpakani kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Meilan wa Haikou katika Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Oktoba 15, 2025. (Xinhua/Yang Guanyu)

Takwimu zilizotolewa na Kituo kikuu cha ukaguzi wa forodhani cha Haikou zimeonesha kuwa, hadi kufikia tarehe 15, Oktoba mwaka huu, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China umeshughulikia safari milioni 2 za abiria wanaoingia na kutoka China, kati yao wasafiri wa kigeni wakichukua asilimia 53.

Mkoa huo kwa muda mrefu umekuwa ukifurahia sera nzuri za abiria wa kigeni kuingia kwa msamaha wa visa nchini China. Wengi wa wageni wanaoingia Hainan wameingia China kutokana na sera ya msamaha wa visa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha