

Lugha Nyingine
Mameya duniani wahamasishwa na mageuzi ya mji wa kauri wa China
Wageni wakihudhuria kikao cha mazungumzo kwenye Mazungumzo ya Mameya Duniani mjini Jingdezhen, Mkoani Jiangxi, mashariki mwa China, Oktoba 19, 2025. (Xinhua/Zhou Mi)
NANCHANG - Katika zama inayotambuliwa zaidi kwa kasi ya kiviwanda na ufanisi wa kidijitali, Jingdezhen, "mji wa kauri" wa China, unachukua njia tofauti: Kuvutia dunia kupitia utamaduni wake wa kauri wa karne nyingi na maono ya kisasa ya mageuzi ya mjini.
Mji huo mdogo katika Mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China ulikuwa mada kuu jana Jumapili kwenye Mazungumzo wa Mameya Duniani ulioleta pamoja mameya, maafisa, wasanii na viongozi wa biashara zaidi 350 ili kutafuta fursa mpya za maendeleo ya miji kupitia utamaduni na utalii.
Alexander Mudrov, mkuu wa Utawala wa Gorodets, Russia, amezungumzia zaidi umuhimu wa uhusiano wa kitamaduni katika kujenga uhusiano wa kimataifa.
"Kabla ya kuzindua miradi ya uchumi, tunahitaji kuwa na uelewa mzuri wa mawazo ya washirika wetu wa kigeni na historia ya kitamaduni," Mudrov amesema, akiongeza: "Hii inahakikisha ushirikiano wa siku za baadaye unategemea msingi thabiti wa urafiki na uhusiano mzuri wa ujirani."
Utamaduni wa kauri kwa muda mrefu umekuwa njia bora ya mazungumzo kati ya ustaarabu mbalimbali. Ikiwa bidhaa ya msingi ya Njia ya Kale ya Hariri, kauri ya Jingdezhen ilikuwa ishara elezi ya kitamaduni ambayo kupitia kwayo dunia ilikuja kuijua China, na China iliifikia Dunia.
Ikijijenga kwenye urithi huo, Jingdezhen imekumbatia mtindo wa maendeleo unaochanganya uhifadhi wa kitamaduni na uhuishaji wa kibunifu.
Ikiwa na wakazi wapatao milioni 1.6, Jingdezhen imeanzisha uhusiano wa ushirikiano na miji zaidi ya 180 katika nchi 72. Bidhaa zake za kauri hufikia nchi na maeneo kadhaa. Maelfu ya wasanii na mafundi wa kauri kutoka nchi zaidi ya 50 huja kuunda bidhaa hapa kama ndege wanaohama.
Wakati wa ziara ya Jingdezhen, Davide Agresti, diwani wa jiji kutoka Faenza, Italia, alishangazwa na mabadiliko ya mji huo, hasa ugeuzaji wa viwanda vya kale vya kauri kuwa maeneo ya utamaduni yenye kusisimua.
"Ninatoka Faenza, pia maarufu kwa kauri." Agresti amesema. "Eneo la kauri la Jingdezhen, kwangu, ni mfano wa namna ya kufanya kazi nzuri na kubwa kwa muda mfupi. Tutajaribu kufanya vizuri kama nyinyi nchini Italia."
Mchanganyo huu wa jadi na uvumbuzi umechochea ukuaji wa sekta ya utalii. Mwaka 2024, Jingdezhen ilipokea watembeleaji wa ndani na nje zaidi ya milioni 60. Wakati wa likizo ya mwaka huu ya China ya Siku ya Taifa na Sikukuu ya Zhongqiu pekee, idadi ya watalii iilizidi milioni 9, ikifikia ukuaji wa tarakimu mbili.
Misri yafunga Jumba la Makumbusho Kuu la Misri kwa ajili ya kufunguliwa rasmi
Mwezi mpevu wavutia kote China wakati wa Sikukuu ya Mbalamwezi ya China
Wanasarakasi wafanya maonyesho katika Eneo la Ulimwengu wa Sarakasi la Wuqiao mjini Cangzhou, China
Sikukuu ya mavuno ya wakulima yaadhimishwa katika Mkoa wa Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma