

Lugha Nyingine
Watalii wa China wasaidia kuchochea utalii wa majira ya baridi katika Mji wa Luxor, Misri
Watalii wa China wakipiga picha wakati wakifanya utalii kwenye Jumba la Hekalu la Karnak mjini Luxor, Misri, Oktoba 5, 2025.(Xinhua/Ahmed Gomaa)
LUXOR, Misri - Ongezeko la watalii wa China linasaidia kustawisha msimu wa utalii wa majira ya baridi wa Mji wa Luxor, likigeuza mji huo wa kale wa Misri kuwa eneo la kutembelewa na watalii kwa mwaka mzima na kukuza uchumi wa nchi hiyo.
Mabadiliko kuelekea safari za kitalii za kujitegemea kunaunda upya mazingira ya utalii ya mji huo wa Luxor.
"Mke wangu na mimi hatukutaka kuja katika kundi la watalii ambalo huratibiwa na wakala wa utalii; tulipanga tu kununua tiketi za ndege na kulipia hoteli na kuja Misri. Hii imetupa uhuru zaidi wa kuzunguka na kutembelea maeneo zaidi," amesema Li Bo, mtalii mwenye umri wa miaka 30 kutoka Beijing, wakati akifanya utalii katika Jumba la Hekalu la Karnak pamoja na mkewe.
Luxor ni "ya kipekee" na "makumbusho kubwa ambayo imejaa vitu vya kale na makumbusho," Li ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua, akiongeza, "unaweza kuhisia historia kila mahali mjini Luxor."
Hali hiyo pia imevutia hadi safari za familia. Wang Changhui, anayeishi na kufanya kazi Dubai, alijumuika na kaka yake Wang Dong anayeishi Shanghai na mama yao kwa safari ya utalii wa kihistoria nchini Misri.
"Hii ni mara yangu ya nane nchini Misri, lakini mara yangu ya kwanza katika Mji wa Luxor. Nimependa utamaduni na historia ya Luxor," amesema Wang Changhui, ambaye aliorodhesha maeneo makuu ya kitalii yakiwemo ya Bonde la Wafalme, Hekalu la Hatshepsut, na Jumba la Hekalu la Karnak.
Wang amesema pia anajivunia kujua kwamba "kuna wanaakiolojia wa China ambao wanasaidia Misri kuhifadhi vitu vya kale katika Hekalu la Montu mjini Luxor."
Wang Dong ameliambia Xinhua shauku yake kwa historia imechochea safari yake hiyo ya kutalii nchini Misri, "ambayo ina historia na ustaarabu uliokita mizizi."
Kwa mujibu wa Ubalozi wa China nchini Misri, watalii wapatao 300,000 Wachina walitembelea Misri mwaka 2024. Mamlaka za Misri zimesema kwamba idadi hiyo inawakilisha ongezeko la asilimia zaidi ya 60 kutoka mwaka 2023.
Mohamed Othman, mwenyekiti wa Kamati ya Kupanua soko la Utalii wa Kitamaduni katika Upper Misri, amethibitisha ongezeko kubwa la watembeleaji wa China.
"Idadi ya watalii wa China inaweza kufikia takriban 400,000 mwaka huu, ikilinganishwa na 300,000 mwaka 2024," Othman amesema, akiongeza kuwa safari za watalii wa China zimekuwa jambo la mwaka mzima.
Ameongeza kuwa Luxor inatayarisha menyu na ishara za habari za maeneo ya kitalii kwa lugha ya Kichina ili kukidhi soko hilo linalokua.
Watalii wa China wakipiga picha wakati wakifanya utalii kwenye Jumba la Hekalu la Karnak mjini Luxor, Misri, Oktoba 5, 2025.(Xinhua/Ahmed Gomaa)
Watalii wa China wakipiga picha wakati wakifanya utalii kwenye Jumba la Hekalu la Karnak mjini Luxor, Misri, Oktoba 5, 2025.(Xinhua/Ahmed Gomaa)
Misri yafunga Jumba la Makumbusho Kuu la Misri kwa ajili ya kufunguliwa rasmi
Mwezi mpevu wavutia kote China wakati wa Sikukuu ya Mbalamwezi ya China
Wanasarakasi wafanya maonyesho katika Eneo la Ulimwengu wa Sarakasi la Wuqiao mjini Cangzhou, China
Sikukuu ya mavuno ya wakulima yaadhimishwa katika Mkoa wa Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma