

Lugha Nyingine
Rwanda na Senegal zasaini makubaliano matano ya ushirikiano ili kuimarisha uhusiano wa pande mbili
Rwanda na Senegal Jumamosi zilisaini makubaliano matano ya pande mbili ili kuimarisha ushirikiano katika maeneo muhimu ya kipaumbele yenye maslahi ya pamoja.
Hafla ya utiaji saini huo ilifanyika Kigali, nchini Rwanda, wakati wa ziara ya kiserikali ya siku tatu ya Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, iliyoanza Ijumaa. Rais wa Rwanda Paul Kagame na Faye walishuhudia utiaji saini huo baada ya kufanya majadiliano kuhusu maeneo yenye umuhimu wa kimkakati.
Makubaliano hayo yanahusu msamaha wa viza kwa wenye hati za kusafiria za kidiplomasia, huduma, na za kawaida, vilevile ushirikiano katika kilimo, afya, huduma za kurekebisha tabia za raia waliofanya jinai na mipango ya Dira ya 2050.
Katika hotuba yake, Rais Kagame amesema viongozi wote wawili wanajali sana mustakabali wa Afrika, hasa jukumu la vijana wake.
Mapema Jumamosi, Rais Faye alitembelea Jumba la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari la Kigali na kutoa heshima kwa waathirika wa Mauaji ya Kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi.
Misri yafunga Jumba la Makumbusho Kuu la Misri kwa ajili ya kufunguliwa rasmi
Mwezi mpevu wavutia kote China wakati wa Sikukuu ya Mbalamwezi ya China
Wanasarakasi wafanya maonyesho katika Eneo la Ulimwengu wa Sarakasi la Wuqiao mjini Cangzhou, China
Sikukuu ya mavuno ya wakulima yaadhimishwa katika Mkoa wa Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma