

Lugha Nyingine
Misri yapendekeza usimamishaji vita wa muda mfupi nchini Sudan ili kufungua njia ya makubaliano ya kudumu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty ametoa wito wa usimamishaji vita wa muda mfupi wa haraka wa kibinadamu nchini Sudan kama hatua ya kwanza kuelekea makubaliano ya kudumu ya kusimamisha vita, akisisitiza upingaji wa Misri wa suluhu yoyote ya kijeshi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo.
Akizungumza jana Jumapili katika kikao cha maendeleo na amani ya Sudan kilichofanyika wakati wa mkutano wa 5 wa Jukwaa la Aswan kwa Amani na Maendeleo Endelevu uliofanyika Aswan, kusini mwa Misri, Abdelatty amesema hakuna suluhu ya kijeshi kwa mgogoro wa Sudan, na kulinda hali ya taifa la Sudan ni jambo muhimu zaidi.
Taarifa iliyotolewa jana Jumapili na Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema, Waziri Abdelatty amesisitiza umuhimu wa kutoingilia mambo ya ndani ya Sudan, kuheshimu uhuru na mamlaka yake kamili, na kudumisha kanuni ya ‘nchi moja, mamlaka moja, na jeshi moja.’
Misri yafunga Jumba la Makumbusho Kuu la Misri kwa ajili ya kufunguliwa rasmi
Mwezi mpevu wavutia kote China wakati wa Sikukuu ya Mbalamwezi ya China
Wanasarakasi wafanya maonyesho katika Eneo la Ulimwengu wa Sarakasi la Wuqiao mjini Cangzhou, China
Sikukuu ya mavuno ya wakulima yaadhimishwa katika Mkoa wa Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma