Ni mambo gani sahihi China inayoyafanya kwa kuongoza siku za baadaye?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 20, 2025

Kila ukifika wakati muhimu wa historia, Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) huwa unaweza kufuata mwelekeo wa historia na mabadiliko ya hali ya mambo, kupanga mikakati ya usahihi, na kuongoza watu wa China kushinda hatari na changamoto na kusonga mbele kwenye safu za mbele za zama zetu. Mkutano wa Nne wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC, ambao unaofanyika wiki hii, utajadili juu ya mapendekezo kuhusu kupanga Mpango wa 15 ya Miaka Mitano (2026-2030) wa China, ukilenga kufanya mpango wa jumla kuhusu utendaji wa pande mbalimbali na kwenye ngazi tofauti juu ya maendeleo ya nchi katika miaka mitano inayofuata, na kusukuma mbele maendeleo makubwa zaidi ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.

Mpango wa miaka mitano ni njia muhimu ya utawala wa nchi wa Chama chetu. Kutoka mpango wa kwanza wa miaka mitano, hadi mpango wa 14 wa miaka mitano, mambo makuu yasiyobadilika ni kuhusu kujenga China kuwa nchi ya kijamaa ya mambo ya kisasa. Ujenzi wa mambo ya kisasa wa China siyo tu umebadilisha hali ya China, bali pia umebadilisha mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa ya dunia inayoendelea, ukisifiwa na wasomi wa kimataifa kuwa mfano wa kuigwa wa mpango wa kimkakati wa muda mrefu.

Ujenzi wa mambo ya kisasa umetatua matatizo mawili magumu yaliyodhaniwa “hayawezekani”: China ilitumia muda wa miongo kadhaa tu imemaliza kupita mchakato wa maendeleo ya viwanda yaliyopita nchi za Magharibi kwa muda wa mamia ya miaka, ikifanya miujiza miwili ya maendeleo ya kasi ya uchumi na utulivu wa jamii wa muda mrefu; ilitumia muda wa miaka minane kuwasaidia idadi ya watu wenye hali ya umaskini karibu milioni 100 wa vijijini kuondokana na umaskini. ikifanya juhudi za kuwezesha zaidi ya watu bilioni 1.4 kuelekea kwa pamoja mambo ya kisasa. Mafanikio hayo mawili ambayo hayajaonekana hapo kabla yameonesha hali tukufu na ya kipekee ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Kwa nini China imeweza kupata mafanikio? Muhimu ni kushika usukani wa kufuata mwelekeo na kuongoza fikra. Kamati kuu ya chama imeweka mpango wa jumla na kutoa mbinu za kufanya kazi usahihi, huku Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China wa Zama Mpya ikijibu kwa njia ya kisayansi swali la China, swali la Dunia, swali la watu na swali la zama, na kutoa uelekezaji wa nadharia na dira ya vitendo. Kushikilia Maendeleo ya sifa bora ya juu ni ukweli wa mambo katika zama mpya. China ikiungwa mkono na nguvu za uzalishaji zenye sifa mpya, inasukuma mbele mabadiliko ya kijani ya pande zote ya uchumi na jamii. Mafanikio dhahiri yamepatikana katika Magari ya nishati mpya (NEVs), viwanda visivyotoa uchafuzi na mfumo wa nishati mbadala, na China imekuwa ikiongoza katika maendeleo ya kijani ya Dunia. Katika miaka 20 iliyopita tangu mawazo ya "milima ya kijani na maji safi ni dhahabu na fedha" yalipotolewa, mawazo hayo yamekita mizizi kwa kina kwenye pande mbalimbali za ujenzi wa ustaarabu wa ikolojia, na kutoa mpango wa China kwa maendeleo endelevu ya dunia.

China ikishikilia hadhi ya mhimili ya wananchi, inahimiza kuunganisha maendeleo ya sifa bora na maisha ya sifa bora. Maendeleo mapya ya miji, ustawishaji wa vijiji na hatua nyingine kadha wa kadha zimekuwa zikiendelea kuboresha maisha ya watu, na pengo kati ya mapato ya wakazi wa mijini na vijijini limekuwa likiendelea kupungua.

China ikishikilia kufanya mpango wa jumla kuhusu maendeleo na usalama, inatumia usimamizi wenye ufanisi wa juu kwa kuhakikisha ujenzi wa mambo ya kisasa unaendelea kwa utulivu. Ujenzi wa utawala kwa mujibu wa sheria unasukumwa mbele kwa hatua madhubuti , huku sheria ya kuhimiza uchumi wa sekta binafsi na sheria ya uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni zikiimarisha mazingira ya biashara.

China ikishikilia ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na inafuata njia ya maendeleo ya amani. Kwa miaka mingi mfululizo China imevutia uwekezaji wa kigeni wa zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 100, na maeneo ya majaribio ya biashara huria, maonesho ya uagizaji bidhaa na majukwaa mengine mbalimbali yanaendelea kupanua ufunguaji mlango.

Baada ya kupita maelfu ya milima na mito, bado tunahitaji kuvuka milima na mito mingi zaidi. Sasa imebaki miaka kumi tu hadi kutimiza kimsingi ujenzi wa mambo ya kisasa, na bado imebaki zaidi ya miaka 20 tu hadi kukamilika kwa ujenzi wa nchi yenye nguvu ya kijamaa ya mambo ya kisasa katika pande zote. Chini ya uongozi imara wa kamati kuu ya chama ambayo Komredi Xi Jinping akiwa kiini chake, kutekeleza kwa pande zote Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China wa Zama Mpya, na kuhamasisha moyo wa kufanya mapambano, hakika siku za baadaye ni za sisi, na hakika ushindi ni wa sisi!

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha