Lugha Nyingine
Hafla ya uzinduzi wa Shirika la Kimataifa la Upatanishi yafanyika Hong Kong

Wageni wakiwa katika picha ya kundi kwenye hafla ya uzinduzi wa Shirika la Kimataifa la Upatanishi (IOMed) mjini Hong Kong, Kusini mwa China, Oktoba 20, 2025. (Xinhua/Zhu Wei)
HONG KONG – Hafla ya uzinduzi wa Shirika la Kimataifa la Upatanishi (IOMed), lenye makao yake makuu katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) wa China, imefanyika mjini Hong Kong jana Jumatatu ambapo tukio hilo limeashiria hatua kubwa katika utatuzi wa migogoro ya kimataifa kwani IOMed ni shirika la kisheria la kimataifa la kati ya serikali mbalimbali lenye dhamira ya kutatua migogoro ya kimataifa kupitia upatanishi.
Hafla hiyo ilikusanya wawakilishi takriban 200 kutoka pande watia saini na waridhiaji wa Mkataba wa Uanzishwaji wa IOMed, vilevile watu kutoka sekta mbalimbali za HKSAR.
Kwenye hotuba yake ya ufunguzi, Hua Chunying, naibu waziri wa mambo ya nje wa China, amesisitiza kwamba kasi ya IOMed kutoka utiaji saini Mkataba hadi kuanzishwa kwake "haijawahi kutokea katika historia ya kuanzisha mashirika ya kimataifa" na inazungumzia ukweli kwamba kuanzishwa kwa IOMed "kunasisitiza msingi wa nyakati zetu na kujibu matarajio ya jumuiya ya kimataifa kwa utatuzi wa migogoro ya kimataifa kwa njia ya amani."
"Maono nyuma ya kuanzishwa kwa IOMed yanawiana sana na yale ya Pendekezo la Utawala Duniani," amesema, huku akiamini kwamba shirika hilo "litatoa msukumo katika ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja" na kuisaidia Hong Kong kuunda hadhi mpya ya "mji mkuu wa upatanishi."
Akihutubia hafla hiyo, John Lee, afisa mtendaji mkuu wa HKSAR, amesema Hong Kong inafurahia vyote faida bora ya China na ile ya kimataifa, na inajivunia desturi iliyoimarishwa ya utekelezaji wa sheria.
Hong Kong inajivunia kuwa "kiunganishi bora" na "kiongeza thamani cha hali ya juu", na inayo heshima ya kutumika kama makao makuu ya Shirika hilo, Lee amesema, akiahidi uungaji mkono kamili wa maendeleo ya IOMed na juhudi za utatuzi wa migogoro.
Teresa Cheng, katibu mkuu mpya aliyechaguliwa wa IOMed, amesema shirika hilo linathamini na kutekeleza mfumo wa pande nyingi, likifanya kazi kama bidhaa yenye manufaa kwa umma duniani na nguzo muhimu katika nyanja ya utatuzi wa amani wa migogoro ya kimataifa.
Wawakilishi kutoka nchi zilizotia mkataba zikiwemo Nicaragua, Venezuela, Jamhuri ya Kongo, Kiribati, Pakistani, Kenya na Dominika walitoa hotuba. Wamesifu umuhimu wa IOMed na kuelezea matarajio yao ya kuchukua jukwaa hilo ili kuhimiza utatuzi wa migogoro ya kimataifa kwa njia ya amani na kutoa mchango katika kujenga utaratibu wa kimataifa ulio wa haki na mantiki zaidi.
Hafla ya kutiwa saini Mkataba wa Kuanzishwa kwa Shirika la Kimataifa kwa ajilil ya Upatanishi (IOMed) ilifanyika Mei 30, 2025, na Mkataba huo ulianza kutumika rasmi Agosti 29, 2025.
Hadi sasa, idadi ya jumla ya nchi zilizotia saini imefikia 37. Nchi nane zimeridhia Mkataba huo, zikiwemo China, Nicaragua, Venezuela, Jamhuri ya Kongo, Kiribati, Pakistan, Kenya na Dominika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



