

Lugha Nyingine
Rais wa Malawi afuta ada za shule, aahidi kumaliza njaa
Rais wa Malawi Peter Mutharika ametangaza elimu bure ya msingi na sekondari kuanzia Januari 2026, wakati huohuo akiwahakikishia wananchi kwamba serikali yake inanunua tani 200,000 za mahindi kutoka nchi jirani ya Zambia ili kutoa chakula kwa watu zaidi ya milioni nne wenye ukosefu wa usalama wa chakula nchini humo.
Mutharika alitoa kauli hiyo juzi Jumapili katika Wilaya ya Thyolo, ambako alikuwa akihudhuria tamasha la kila mwaka la utamaduni kwa ajili ya watu wa kabila la Walhomwe.
Kiongozi huyo wa Malawi ambaye aliapishwa Oktoba 4 kuwa rais wa saba wa nchi hiyo kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa Septemba 16, ameeleza kuwa elimu ni muhimu kwa maendeleo ya taifa, akihimiza wazazi na walezi nchini humo kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anahudhuria shule.
Kuhusu suala la usalama wa chakula, rais huyo amewahakikishia Wamalawi wote walioathiriwa na njaa kuwa kila kitu kimeshapangwa na kwamba amemtuma waziri wa kilimo wa nchi hiyo kwenda Zambia kukamilisha makubaliano ya kupatiwa mahindi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma