Lugha Nyingine
Shughuli za utalii za ndani ya China zaongezeka kwa asilimia 18 katika robo tatu za kwanza

Watalii wakifanyiwa utaratibu wa kuingia na kutoka kwenye hoteli katika Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Wali ya Lingshui, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Oktoba 18, 2025. (Xinhua/Guo Cheng)
BEIJING – Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China jana Jumanne zimeonyesha kuwa, safari za watu za utalii ndani ya China karibu zimefikia mara bilioni 5 katika robo tatu za kwanza za mwaka, zikifikia ongezeko la asilimia 18 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.
Matumizi ya jumla ya watu waliofanya utalii ndani ya China yalifikia yuan trilioni 4.85 (dola za kimarekani karibu bilioni 684) katika muda wa miezi tisa iliyopita, ikiongezeka kwa asilimia 11.5 kuliko kipindi kama hicho mwaka 2024.
Wakazi wa mijini wameendelea kuwa kichocheo kikuu cha utalii wa ndani wa China. Walifanya utalii karibu kwa mara bilioni 3.8, huku matumizi ya jumla yakifikia yuan trilioni 4.05, takwimu hizo zinaonyesha.
Hasa, idadi ya wakazi wa vijijini waliofanya utalii ndani ya China iliongezeka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, na ongezeko la matumizi yao limefikia asilimia 24.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



