Lugha Nyingine
Makamu Rais wa China akutana na Spika wa Baraza la Juu la Jimbo la Oregon, Marekani

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Rob Wagner, Spika wa Baraza la Juu la Jimbo la Oregon la Marekani, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Oktoba 21, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)
BEIJING - Makamu Rais wa China Han Zheng amekutana na Rob Wagner, Spika wa Baraza la Juu la Jimbo la Oregon la Marekani, jana Jumanne mjini Beijing, akisema kuwa maafikiano muhimu yamefikiwa kati ya viongozi wa nchi hizo mbili wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu yaliyofanyika tangu mwanzoni mwa mwaka huu, na kwamba kwa kuwa zina maslahi mapana na matarajio mazuri ya ushirikiano, China na Marekani zinapaswa kuwa washirika na marafiki.
"China inatumai kuwa Marekani itashirikiana nayo katika kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na kunufaishana, na kutafuta njia sahihi kwa nchi hizo mbili kubwa kupatana katika zama mpya, zikilenga kunufaisha pande hizo mbili na dunia kwa ujumla." Han amesema.
"Oregon imekuwa ikidumisha uhusiano wa kirafiki na wa ushirikiano na China kwa muda mrefu," Han amesema, akiongeza kuwa, China inatumai kuwa Spika wa Baraza la Juu la Jimbo la Oregon Wagner na maseneta wenzake wataendelea kuimarisha mawasiliano kati ya pande hizo mbili, kuzidisha uhusiano kati ya watu na watu na kubeba jukumu la kupigiwa mfano katika kuhimiza ushirikiano wa serikali za mitaa kati ya China na Marekani.
Kwa upande wake Wagner ameelezea matumaini yake kwa mafanikio ya mkutano wa nne wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China, na kusema kuwa ushirikiano kati ya Marekani na China katika ngazi ya serikali za mitaa ni muhimu sana, akiongeza kuwa jimbo la Oregon limepitisha mswada wa kuendelea kuimarisha ushirikiano wake wa kirafiki na China.

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Rob Wagner, Spika wa Baraza la Juu la Jimbo la Oregon la Marekani, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Oktoba 21, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



