

Lugha Nyingine
Waziri wa Zimbabwe apongeza uwekezaji wa China katika kuhimiza uzalishaji wa saruji
Waziri wa Habari, Uenezi, na Huduma za Utangazaji wa Zimbabwe Bw. Jenfan Muswere amepongeza uwekezaji unaoongezeka kutoka China kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kuzalisha saruji wa nchi hiyo.
Akizungumza jana Jumanne kwenye mkutano na wanahabari wa baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri la Serikali ya Zimbabwe uliofanyika mjini Harare, waziri huyo amesema kampuni za China zimewekeza dola za Kimarekani zaidi ya bilioni moja kwenye sekta ya saruji nchini Zimbabwe katika mwaka uliopita.
Amesema kuongezeka huko kwa uwekezaji wa China kunaendana na jitihada za serikali za kufufua sekta ya viwanda na kuharakisha ukuaji wa viwanda.
Muswere amebainisha kuwa Mpango wa Ujenzi Upya wa Viwanda na Ukuaji wa Zimbabwe ambao ni mfumo wa mpito kati ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda ya Taifa iliyoisha muda wake na sera mpya itakayotolewa, umeweka msingi imara kwa ajili ya ajenda ya uendelezaji wa viwanda nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma