Botswana yatoa wito kwa vijana na jumuiya za wenyeji kuchangamkia fursa za madini ili kubadilisha muundo wake wa kiuchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 22, 2025

Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu wa Botswana Noah Salakae akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Madini ya Botswana mjini Gaborone, Botswana, Oktoba 21, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu wa Botswana Noah Salakae akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Madini ya Botswana mjini Gaborone, Botswana, Oktoba 21, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE - Serikali ya Botswana na taasisi za kifedha za nchi hiyo zimetoa wito kwa vijana wa nchi hiyo na jumuiya za wenyeji kufuatilia kikamilifu ushirikiano na fursa za mambo ya kifedha ili kushiriki katika sekta ya madini na kusaidia kujenga mustakabali wa siku za baadaye wa nchi hiyo.

Akitoa hotuba kuu kwa niaba ya Rais Duma Boko jana Jumanne kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Madini ya Botswana, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais wa Botswana Moeti Mohwasa amezungumzia dira ya serikali ya kujenga uchumi wa madini unaojitegemea na wa sekta mbalimbali, kuanzia uchimbaji madini hadi mageuzi ya ongezeko la thamani.

Ameelezea mabadiliko thabiti ya Botswana kutoka kuwa muuzaji nje mkuu wa madini ghafi hadi kuwa kiongozi wa kikanda katika utafutaji, kunufaika na madini, na ukuaji endelevu wa kisekta, akisisitiza mchango wa teknolojia, uvumbuzi, data, na uchumi unaowezeshwa kidigitali.

Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu Noah Salakae amesema kuwa utajiri wa madini wa Botswana ni zaidi ya almasi pekee, akirejelea rasilimali ambazo hazijatumiwa zikiwemo za makaa ya mawe, shaba, nikeli, dhahabu, fedha, manganese, urani, ore ya chuma, na vitu vya madini adimu.

"Rasilimali hizi ni muhimu kwa mabadiliko ya kimataifa kuelekea nishati mbadala na teknolojia ya hali ya juu," Salakae amesema, akiyaelezea madini ya Botswana kuwa siyo tu bidhaa zinazouzwa nje ya nchi lakini kuwa ni "funguo kwa mageuzi ya kiviwanda," na kuhimiza nchi hiyo kujiweka katika nafasi ya kuwa kituo cha kikanda kwa uchimbaji madini wenye kuwajibika na kunufaisha wenyeji.

Amehimiza wananchi kuchunguza ushirikiano, ufadhili, na uungaji mkono wa kiufundi ili kutumia kikamilifu leseni zao za uchimbaji au utafutaji madini, hasa kupitia ushirikiano na benki na taasisi za fedha ili "kuchunguza machaguo ya ufadhili bunifu na kampuni za ubia."

Maonyesho hayo ya siku tatu ya Madini ya Botswana yanatarajiwa kuvutia washiriki wapatao 10,000, wakiwemo mawaziri, viongozi wa biashara, wajasiriamali, wafadhili, wachimbaji wadogo na wanafunzi.

Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu wa Botswana Noah Salakae akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Madini ya Botswana mjini Gaborone, Botswana, Oktoba 21, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu wa Botswana Noah Salakae akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Madini ya Botswana mjini Gaborone, Botswana, Oktoba 21, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha