Lugha Nyingine
Mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho la Louvre la Paris, Ufaransa akiri kushindwa kwa ulinzi wa usalama, apendekeza hatua mpya
Watalii wakionekana mbele ya Piramidi ya Jumba la Makumbusho la Louvre mjini Paris, Ufaransa, Oktoba 22, 2025. (Xinhua/Zhang Baihui)
PARIS - Mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho la Louvre mjini Paris, Ufaransa Laurence des Cars amekiri kushindwa katika mfumo wa kurekodi matukio kwa nje wa jumba hilo la makumbusho na ametangaza mfululizo wa hatua mpya za ulinzi wa usalama.
Akizungumza mbele ya Baraza la Juu la Bunge la Ufaransa jana Jumatano, des Cars amesema ufikiaji wa kamera za ufuatiliaji na udhibiti (CCTV) kwa nje ya jumba hilo la makumbusho hautoshi na wizi wa vito siku ya Jumapili umefichua "maeneo dhaifu" kadhaa.
"Tunakabiliwa na kushindwa vibaya katika jumba la Louvre, ambapo kutokana na hilo ninachukua jukumu langu ya kuwajibika," amesema, akiongeza kwamba ameomba kujiuzulu, lakini waziri wa utamaduni amekataa ombi hilo.
Watu wa ulinzi wa usalama wakiwa kwenye doria nje ya Jumba la Makumbusho la Louvre mjini Paris, Ufaransa, Oktoba 22, 2025. (Xinhua/Zhang Baihui)
Des Cars ameeleza hatua kadhaa za kuimarisha ulinzi wa usalama, ikiwemo kuimarisha ulinzi wa pembeni na vizuizi vya kuzuia magari, kupanua na kuboresha mifumo ya kufuatilia na kurekodi matukio katika jumba hilo la makumbusho, na kuomba Wizara ya Mambo ya Ndani kuanzisha kituo cha polisi ndani ya jumba hilo la makumbusho.
Wakati huo huo, ametetea mpango wa ulinzi wa usalama uliopo wa jumba hilo la makumbusho wenye gharama ya euro milioni 80 (dola za Kimarekani milioni 92.89), akikataa ripoti ya hivi karibuni ambayo ilirejelea "kuahirishwa mara kwa mara" katika utekelezaji wa mpango huo.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa wito wa kuharakishwa kwa kupandisha daraja la ulinzi wa usalama wa jumba hilo la Louvre kwenye mkutano wa baraza la mawaziri jana Jumatano.
Jumba hilo la makumbusho lilifunguliwa tena kwa watembeleaji jana Jumatano asubuhi, siku tatu baada ya wizi wa kustaajabisha wa vito vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya euro milioni 88 (dola za Kimarekani milioni 102).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



