Lugha Nyingine
Sudan yafungua tena Uwanja wa Ndege wa Khartoum uliofungwa kwa miaka miwili na nusu kwa usafiri wa ndege nchini
KHARTOUM - Sudan imetangaza jana Jumatano kwamba itafungua tena Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum kwa usafiri wa ndege nchini, ikimaliza usitishaji wa huduma ya usaifiri wa ndege kwa karibu miaka miwili na nusu, ingawa hivi karibuni uwanja huo wa ndege uliwahi kushambuliwa kwa droni.
"Ndege ya Shirika la Ndege la Badr imetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum, ikimaanisha kufunguliwa tena kwa uwanja huo na kuanza kwa usafiri wa ndege kutoka mji mkuu baada ya kusitishwa kwa muda mrefu," Wizara ya Utamaduni, Habari, na Utalii ya Sudan imesema katika taarifa.
Taarifa yake kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook imesema, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum umesema kuanzishwa tena kwa usafiri wa ndege ni "hatua muhimu katika ufufukaji wa sekta ya usafiri kwenye anga ya Sudan, ikitandika njia ya kurejea hatua kwa hatua kwa usafiri wa anga katika kipindi kijacho."
Uwanja huo wa ndege, ulioko katikati mwa Khartoum, ulikuwa umeshambuliwa kwa droni siku ya Jumanne na Jumatano asubuhi.
Mapema siku hiyo, wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) walidai kuhusika na shambulizi la Jumatano dhidi ya Khartoum.
Uwanja huo wa ndege ulikuwa sehemu moja kati ya maeneo yaliyoshambuliwa kwanza na RSF wakati vita vilipozuka Aprili 15 , 2023, na ulipatwa na uharibifu mkubwa wakati wa kipindi cha mwanzo wa vita.
Mamlaka zimefanya kazi ya kukarabati uwanja huo wa ndege baada ya jeshi kurejesha udhibiti kamili wa Jimbo la Khartoum mwezi Mei.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



