Afrika Kusini yakaribisha uamuzi wa Zimbabwe wa kuondoa marufuku ya kuagiza mahindi

(CRI Online) Oktoba 23, 2025

Waziri wa Kilimo wa Afrika Kusini John Steenhuisen amekaribisha uamuzi wa Zimbabwe wa kuondoa marufuku ya kuagiza mahindi na nafaka nyingine kutoka nje ya nchi, akiuelezea kuwa ni hatua muhimu kuelekea utulivu wa kiuchumi na usalama wa chakula katika eneo hilo.

Katika taarifa yake ya Jumatano, Steenhuisen amesema mabadiliko hayo ya sera yanaakisi kurejea kwa kanuni bora za kiuchumi ambazo ni muhimu kwa ustawi na utulivu wa eneo la Kusini mwa Afrika.

Steenhuisen amebainisha kuwa kuondolewa kwa marufuku hiyo kutasaidia kuleta utulivu wa bei ya mahindi na kusaidia uwekezaji wa biashara ya kilimo katika eneo lote.

Wizara ya Kilimo ya Afrika Kusini imesema bado imedhamiria kushirikiana na washirika wote wa kanda hiyo ili kukuza biashara ya haki, wazi na yenye ufanisi katika mazao ya kilimo, ambayo imeielezea kuwa msingi wa ukuaji endelevu na kupunguza umaskini kusini mwa Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha