Kampuni ya uchimbaji wa uranium ya China yachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Mkoa wa Erongo, Namibia

(CRI Online) Oktoba 23, 2025

Taasisi ya Swakop Uranium iliyoanzishwa kwa uwekezaji wa China imeonesha dhamira ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Mkoa wa Erongo nchini Namibia kupitia kupanua mpango wake wa kitaifa wa muda mrefu unaolenga kuleta maisha endelevu.

Taasisi hiyo ilifanya hafla Jumanne usiku, ikiashiria kuanza kwa awamu ya pili ya Mradi wa Hope Farm, na kuchangia mbuzi na kondoo 1,008 wenye thamani ya dola milioni 3 za Namibia (sawa na dola za Kimarekani laki 1.73) kwa wanufaika 48 wa mkoa huo.

Awamu ya kwanza ya mradi huo ilianzishwa mwezi Julai, na kutoa mifugo 630 kwa wanufaika 30. Kwenye awamu ya pili, wanufaika wapya 18 wamepewa mifugo 378, wakiwakilishwa na vyama vya ushirika vya Nderurua, Omkhaibasen, na Okongava-Ondjeombaranga.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha