

Lugha Nyingine
Uzuri wa Majira: Kushuka kwa Jalidi
Hamjambo! Mimi ni Sisi, mpenda kutalii. Wakati ukungu wa asubuhi unapoteleza juu ya milima pamoja na baridi kidogo, na majani kwenye matawi kugeuka kuwa ya rangi ya dhahabu na nyekundu, tunakaribisha Shuangjiang, au Kushuka kwa Jalidi – kipindi cha mwisho cha majira ya mpukutiko katika kalenda ya Kilimo ya China. Kwa sasa, niko katika Kijiji cha Hongcun, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China. Njoo ujumuike nami tunapotembelea katika kijiji hiki cha kale kilichofunikwa na jalidi, na kuhisi unyororo wa kina wa msimu huu wakati "hewa inakua shwari na umande kugeuka kuwa jalidi."
Kushuka kwa Jalidi kunakigeuza kijiji cha Huizhou kuwa picha ya kuchorwa. Kunapopambazuka, Ziwa Nanhu limetanda kwenye ukungu, matawi ya miti kando ya ufukwe yamejaa vumbi na jalidi kali nyeupe. Mwanga wa jua unapopenya mawingu, chembechembe za jalidi humeta kwa ulaini, zikitawanya mawimbi ya dhahabu katika ziwa hilo. Unapotembea kwenye njia zilizojengwa kwa mawe, utaona mimea ya crimson maple iking’ara kwenye lango la kijiji, majani yake yaliyoanguka yakiwa yamezagaa kwenye kuta zilizopakwa chokaa na ngazi za mawe, kama michirizi kutoka kwenye ubao wa mchoraji. Hali ya Kushuka kwa Jalidi hutanda katika ukarimu wa kila siku wa kijiji hicho: viazi vitamu vilivyokaushwa huning’inia kwenye kuta, utamu wake laini unaingizwa na ladha ya jua na udongo, "akiba ya utamu" kwa ajili ya majira ya baridi yajayo.
Kwa upande mwingine wa dunia, wakati huu wa mwishoni mwa majira ya mpukutiko huchukua mvuto wake wenyewe. Huko Toscany, Italia, ni msimu wa mavuno ya mizeituni. Wakulima husogea kwenye vichaka, wakichuna mizeituni ili kuikandamiza kwenye mafuta freshi. Wanafurahia mkate wa joto unaotoka moja kwa moja kwenye oveni, ladha rahisi lakini ya kipekee sana ya majira ya mpukutiko.
"Jalidi inaposhuka, anga hugeuka kuwa safi, na majira ya mpukutiko hupeperushwa kuelekea magharibi kwa upepo." Kushuka kwa Jalidi kunaashiria mwisho wa majira ya mpukutiko na mwanzo wa majira ya baridi, kukibeba hali ya mabadiliko ya kimsimu na furaha ya maisha. Je, Kushuka kwa Jalidi kunaonekanaje mahali ulipo? Toa simulizi zako za majira ya mpukutiko, na tufurahie pamoja uzuri wa mwisho wa majira ya mpukutiko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma