Mkutano wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya CPC wamalizika, wapitisha mapendekezo ya Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 24, 2025

Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye pia ni Rais wa China, akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC mjini Beijing, China. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING - Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano wake wa nne wa wajumbe wote mjini Beijing kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi wiki hii ambapo watu waliohudhuria kwenye mkutano huo wamejadili na kupitisha Mapendekezo ya Kamati Kuu ya CPC ya kupanga Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii, taarifa ya kikao hicho iliyotolewa jana Alhamisi imesema.

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC iliongoza mkutano huo, na Xi Jinping, katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, alitoa hotuba muhimu, taarifa hiyo imesema.

Watu waliohudhuria kwenye mkutano huo walisikiliza na kujadili ripoti iliyotolewa na Xi kuhusu kazi ya Ofisi ya Siasa. Xi pia alitoa hotuba ya ufafanuzi kuhusu mswada wa mapendekezo.

Kwenye mkutano huo , Kamati Kuu ya CPC imethibitisha vya kutosha kazi ya Ofisi hiyo ya Siasa tangu mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC.

Taarifa hiyo imesema, China kwa hivi sasa iko katika kipindi muhimu cha kukamilisha malengo na majukumu makuu ya Mpango wa 14 wa Miaka Mitano.

Watu waliohudhuria kwenye mkutano huo wametoa tathmini nzuri ya mafanikio makubwa ya maendeleo ya China wakati wa kipindi cha Mpango wa 14 wa Miaka Mitano (2021-2025), na kipindi hiki ni kipindi chenye umuhimu mkubwa na kisicho cha kawaida katika historia ya maendeleo ya China.

Kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) kitafanya kazi muhimu sana kwa kuimarisha msingi na kusukuma mbele maendeleo ya mambo mbalimbali, na kutandika njia kwa ajili ya kufikia kimsingi mambo ya kisasa ya kijamaa ifikapo mwaka 2035, na hivyo kitakuwa kiungo muhimu kati ya yaliyopita na yajayo, taarifa hiyo inasema.

Taarifa hiyo imedhihirisha kwamba kwa hivi sasa, China bado iko kwenye kipindi cha maendeleo ambapo fursa za kimkakati zinakuwepo pamoja na hatari na changamoto, wakati huohuo hali ya kutokuwa na uhakika na mambo yasiyotarajiwa yanaongezeka.

Katika mkutano huo, Kamati Kuu ya CPC imethibitisha kanuni zifuatazo za mwongozo wa maendeleo ya uchumi na jamii wakati wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano: Kudumisha uongozi wa Chama wa pande zote; kuweka watu katika kipaumbele cha juu; kuhimiza maendeleo ya sifa bora ya juu; kuendeleza mageuzi kwa kina na kwa pande zote; kuhimiza kufanya kazi kwa ushirikiano kati ya soko lenye ufanisi na serikali inayofanya kazi vizuri; na kuhakikisha umuhimu wa pamoja wa maendeleo na usalama.

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ikiongoza mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC mjini Beijing, China. (Xinhua/Ding Haitao)

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ikiongoza mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC mjini Beijing, China. (Xinhua/Ding Haitao)

Xi Jinping, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi wakihudhuria kwenye mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) mjini Beijing. (Xinhua/Shen Hong)

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ikiongoza mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC mjini Beijing. (Xinhua/Li Xiang)

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ikiongoza mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC mjini Beijing. (Xinhua/Li Xiang)

Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ikifanya mkutano wake wa nne wa wajumbe wote mjini Beijing. (Xinhua/Li Xiang)

Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ikifanya mkutano wake wa nne wa wajumbe wote mjini Beijing. (Xinhua/Li Xiang)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha