Lugha Nyingine
Indonesia na Brazil zasaini Makubaliano ya Maelewano ili kusukuma mbele ushirikiano wa pande mbili

Rais wa Indonesia Prabowo Subianto (kulia) na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva wakihudhuria mkutano wa pamoja na waandishi wa habari katika Ikulu ya Merdeka mjini Jakarta, Indonesia, Oktoba 23, 2025. (Picha/CFP)
JAKARTA - Indonesia na Brazil zimesaini mfululizo wa nyaraka za makubaliano ya maelewano (MoUs) jana Alhamisi ili kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, zikiwemo za nishati, madini, kilimo, sayansi na biashara, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Sekretarieti ya Rais wa Indonesia.
Hafla ya kutia saini nyaraka hizo za makubaliano, iliyoshuhudiwa na Rais wa Indonesia Prabowo Subianto na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, imefanyika katika Ikulu ya Merdeka mjini Jakarta wakati wa ziara ya kiserikali ya Rais Lula.
"Leo (jana Alhamisi), tutasaini makubaliano na maelewano muhimu manne, na natumai huu ni uthibitisho kwamba tunafanya kazi haraka. Nina imani kwamba katika siku zijazo, tutapata matokeo makubwa zaidi," amesema Rais Prabowo kwenye mkutano wa pande mbili.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya rais huyo, nyaraka hizo za makubaliano zimesainiwa kati ya taasisi kadhaa za serikali na mashirika ya biashara kutoka nchi zote mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



