Hifadhi ya Kijiolojia ya Dunia nchini Tanzania yafufuliwa kwa msaada wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 24, 2025

Wahandisi wa China kutoka Kituo cha Tianjin cha Idara ya Utafiti wa Kijiolojia ya China wakifanya utafiti wa kimazingira katika hifadhi ya kijiolojia. (Picha imetolewa kwa China Daily/kuchapishwa na People’s Daily Online)

Wahandisi wa China kutoka Kituo cha Tianjin cha Idara ya Utafiti wa Kijiolojia ya China wakifanya utafiti wa kimazingira katika hifadhi ya kijiolojia. (Picha inatoka China Daily)

Saa 9 alasiri Septemba 2023, watu zaidi ya 50, walikuwa wamekusanyika kwenye volkano ya Ol Doinyo Lengai kaskazini mwa Hifadhi ya Kijiolojia ya Dunia ya Ngorongoro-Lengai mkoani Arusha, Tanzania.

Raia hao wa China na Tanzania walikuwa wamepanda kwa zaidi ya saa saba. Kazi yao ilikuwa ni utafiti wa urithi wa kijiolojia wa shimo la volkano, ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi upya uliofanywa na serikali ya China ili kusaidia katika maendeleo ya hifadhi hiyo ya kijiolojia ya dunia ya kwanza na ya pekee ya Tanzania.

Volkano ya Ol Doinyo Lengai ikikaribia kujitokeza kwenye Hifadhi ya Kijiolojia Duniani ya Ngorongoro-Lengai mjini Arusha, Tanzania. (Picha imetolewa kwa China Daily/kuchapishwa na People’s Daily Online)

Volkano ya Ol Doinyo Lengai ikionekana kwenye Hifadhi ya Kijiolojia ya Dunia ya Ngorongoro-Lengai mjini Arusha, Tanzania. (Picha inatoka China Daily)

Ikipatikana kaskazini mashariki mwa Tanzania, hii ni hifadhi pekee ya kijiolojia ya dunia katika Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwa na sifa za kijiolojia zenye umuhimu wa kimataifa. Inajulikana zaidi kwa Bonde la Ngorongoro, volkano hai ya Ol Doinyo Lengai na maeneo ya paleontolojia ya Olduvai Gorge, ikifungua milango kwa utalii, uhifadhi, elimu na utafiti.

Mwaka 2018, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) liliiidhinisha kuwa hifadhi ya kijiolojia ya dunia, ikichukua eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba takriban 12,000 katika wilaya za mkoa huo wa Arusha za Ngorongoro, Karatu na Monduli. Hata hivyo, kutokana na matatizo kama vile miundombinu duni ya kimsingi, uchache wa taarifa za watalii na maudhui yasiyotosheleza ya uelezeaji wa kisayansi, hifadhi hiyo ya kijiolojia ilipokea onyo la njano kutoka UNESCO mwaka 2022 na ilipewa kipindi cha miaka miwili cha marekebisho na kufanyiwa tathmini upya.

China iliingilia kusaidia katika wakati huo muhimu. Wakati wa ziara ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan nchini China mwezi wa Novemba mwaka huo huo, yeye na Rais wa China Xi Jinping walihudhuria hafla ya utiaji saini mradi unaosaidiwa na China unaolenga kumaliza changamoto hizo zinazokabili hifadhi hiyo ya kijiolojia.

Ukiungwa mkno na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kimataifa la Wizara ya Biashara ya China, Ubalozi wa China nchini Tanzania na Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya China, mradi huo umejumuisha vyote usaidizi wa kiufundi kutoka Kituo cha Tianjin cha Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya China na miundombinu ya kwenye hifadhi inayofanyiwa kazi na Kampuni ya 25 ya Kundi la Kampuni za Shirika la Reli la China.

Wataalam wa timu ya utafiti ya China wakiangalia sampuli ya jiwe kwenye hifadhi ya kijiolojia. (Picha imetolewa kwa China Daily/kuchapishwa na People’s Daily Online)

Wataalam wa timu ya utafiti ya China wakiangalia sampuli ya jiwe kwenye hifadhi ya kijiolojia. (Picha inatoka China Daily)

Kwa kipindi cha mwaka zaidi ya mmoja, timu hiyo ilikamilisha uchunguzi wa kina wa hifadhi hiyo ya kijiolojia, ambao ulijumuisha kuchunguza maeneo ya urithi wa kijiolojia, vyanzo vya maji ya chini ya ardhi na sifa za tabaka za miamba ya muundo wa volkano, vilevile uelezeaji wa data za kijiolojia za kuhisiwa kwa mbali.

Kwa sasa, alama karibu 300, zikiwemo za uelezeaji, za kuonesha uelekeo na tahadhari za usalama, zimewekwa kwenye hifadhi hiyo ya kijiolojia - zote kwa Kiingereza, Kiswahili na Kichina. Mfumo wa kuelezea eneo hilo pia upo, ukitoa maudhui ya kuelezea kwa maeneo muhimu katika lugha saba za Kiingereza, Kiswahili, Kichina, Kifaransa, Kijerumani, Kihispania na Kiarabu.

Hifadhi hiyo ya kijiolojia hutoa makazi yanayostawi yenye maji na mbuga za kutosha kwa wanyama pori 300,000, ikiunda mfumo wa ikolojia wa savanna ya kitropiki unaojitegemea wenyewe.

Wu Xingyuan, mjumbe wa mradi huo kutoka Kituo cha Tianjin amesema, ili kulinda wanyama hao, njia ndogo za udongo zimehifadhiwa vizuri ili kuzuia uharibifu wa kwato zao. Aidha, kazi lazima ikome, na kila mtu lazima awe ameondoke ifikapo saa 11 jioni, hivyo kurudisha eneo hilo kwa wanyamapori.

"Sifa nyingine ya kipekee ya hifadhi hii ya kijiolojia ni kwamba ni nyumbani kwa wakazi karibu 400,000, huku wengi wao wakiwa Wamasai," Wu ameongeza.

Ili kuheshimu watu hawa wenyeji ambao wamekuwa wakiishi hapa kwa vizazi vingi, timu hiyo imeandaa ziara ambapo watembeleaji hifadhi hiyo wanaweza kujichangamanisha katika mtindo wa maisha wa Wamasai, kula vyakula vyao vya kijadi na kucheza pamoja nao.

Twiga wakiwa kwenye Hifadhi ya Kijiolojia Duniani ya Ngorongoro-Lengai. (Picha imetolewa kwa China Daily/Kuchapishwa na People’s Daily Online)

Twiga wakiwa kwenye Hifadhi ya Kijiolojia Duniani ya Ngorongoro-Lengai. (Picha inatoka China Daily)

Aidha, timu hiyo imetekeleza programu ya mafunzo ya vipaji ya mwezi mmoja kwa wakazi wenyeji, ikiwapa maarifa ya kina kuhusu hifadhi hiyo ya kijiolojia.

Juhudi katika kazi hizo ngumu zilizaa matunda wakati UNESCO ilipoithibitisha tena kwa mafanikio hifadhi hiyo mwezi Desemba mwaka jana, na mradi huo uko njiani kukamilika ifikapo mwezi wa Novemba.

Zhang Zhonghui, mhandisi mwandamizi na mtaalam wa Jumuiya ya Kijiolojia ya China, ameuelezea mradi huo wa msaada wa kigeni kuwa ni "mfano bora wa ushirikiano wa kimataifa".

"Mradi huo si tu umeisaidia Tanzania kuunda kundi la bidhaa na shughuli za kipekee za kitamaduni na utalii lakini pia umefanikisha uwezeshaji wa muda mrefu kupitia mafunzo ya wafanyakazi na maboresho katika maisha ya wenyeji," Zhang Zhonghui amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha