Lugha Nyingine
Rais Xi na mwenzake wa Finland watumiana salamu za pongezi kwa maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Finland Alexander Stubb jana Jumanne wametumiana salamu za pongezi kwa maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ambapo Rais Xi amesema, Finland ni "nchi inayopendeza ya maziwa elfu" na ni moja ya nchi za kwanza za Ulaya kusaini makubaliano ya biashara ya kati ya serikali na China.
"Katika miaka 75 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano kati ya China na Finland umevuka tofauti katika mfumo wa jamii na itikadi, na umeshinda majaribu katika mabadiliko ya hali ya kimataifa, huku ushirikiano umeendelea kwa kina katika sekta za siasa, uchumi, na biashara, mawasiliano kati ya raia, na mambo ya utamaduni," Xi amesema.
Rais Xi amesema, Rais Stubb kwa mafanikio alifanya ziara ya kiserikali nchini China Oktoba mwaka uliopita, ambapo waliweka pamoja dira ya ukuzaji wa aina mpya ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano kati ya China na Finland unaoelekea siku za baadaye.
Rais Xi amesema anatilia maanani sana ukuaji wa uhusiano kati ya China na Finland, na anapenda kushirikiana na Rais Stubb katika kurithisha urafiki wa jadi wa nchi hizi mbili, kuanzisha sekta mpya katika ushirikiano wa pande mbili, na kusukuma mbele dunia ya ncha nyingi yenye usawa na utaratibu na utandawazi wa uchumi wa dunia wenye manufaa na ulio jumuishi kwa wote.
Kwa upande wake, Stubb amesema, uhusiano kati ya Finland na China ni wa karibu na wenye msingi imara, katika miaka 75 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano wa pande mbili umeendelea kwa hatua madhubuti huku ushirikiano ukipanuka siku hadi siku.
Amesema kuwa wakati wa ziara yake ya kwanza ya kiserikali nchini China mwezi Oktoba wa mwaka jana, pande hizo mbili zilitangaza Mpango wa Utendaji wa Pamoja kati ya China na Finland kuhusu Kuhimiza Aina Mpya ya Uhusiano wa Wenzi wa Ushirikiano Unaoelekea Siku za Baadaye 2025-2029.
“Jumuiya ya kimataifa inaamini umuhimu wa China ikiwa mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,” amesema, akiongeza kuwa anatarajia kuendeleza mazungumzo na Rais Xi kuhusu masuala ya pande mbili na ya kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



