Lugha Nyingine
Ajali ya ndege ya kitalii nchini Kenya yasababisha vifo vya watu 11
 (CRI Online) Oktoba 29, 2025
		
		Ajali ya ndege iliyotokea karibu na pwani ya Kenya mapema jana Jumanne imesababisha vifo vya watalii 10 kutoka Ulaya na rubani mmoja mwenyeji.
Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kutoka hoteli moja ya ufukweni ya Diani kuelekea kwenye uwanja wa ndege wa Hifadhi ya Taifa ya Maasai Mara.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa Ndege za Kiraia ya Kenya (KCAA) imesema ndege hiyo ilikuwa imebeba wataii wanane kutoka Hungary, Wajerumani wawili na rubani mmoja wa Kenya, ambao wote wamefariki dunia kwenye ajali hiyo, na kinachofanyika sasa ni kutoa msaada wote kwa familia za abiria hao waliofariki.
Kamishna wa Kaunti ya Kwale Bw. Stephen Orinde amesema ndege hiyo ilianguka umbali wa kilomita 10 hivi kutoka mji wa Kwale baada ya kuruka kutoka Diani.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
	Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
	people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



