China yajenga kilomita 75,000 za barabara za vijijini katika robo tatu za kwanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 29, 2025

Picha iliyopigwa Mei 9, 2024 ikionyesha barabara ya kijijini baada ya kuboreshwa katika Wilaya ya Yuanshi ya Mji wa Shijiazhuang, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China. (Xinhua/Yang Shiyao)

Picha iliyopigwa Mei 9, 2024 ikionyesha barabara ya kijijini baada ya kuboreshwa katika Wilaya ya Yuanshi ya Mji wa Shijiazhuang, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China. (Xinhua/Yang Shiyao)

HANGZHOU - China ilijenga na kuboresha kilomita 75,000 za barabara za vijijini katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, ikikamilisha asilimia 75.4 ya lengo la mwaka, takwimu rasmi zilizotolewa jana Jumanne na Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ya China zinaonesha.

Takwimu hizo zimetolewa kwenye shughuli za mada kuhusu barabara za vijijini katika Mji wa Quzhou, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, zikionesha maendeleo ya China katika kuimarisha miundombinu ya vijijini.

Wizara hiyo imesema kuwa thamani ya jumla ya uwekezaji wa mali zisizohamishika za barabara za vijijini ilifikia yuan zaidi ya bilioni 275.3 (Dola za Kimarekani karibu bilioni 38.8) katika kipindi cha miezi tisa.

Ofisa kutoka Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ya China amesema kuwa, shughuli hizo zimehusisha na shughuli ya kutembelea katika vijiji, vituo vya viwanda na maeneo ya utalii wa kitamaduni, na kuonyesha namna mitandao bora ya barabara inavyochochea ustawishaji wa vijiji na kuongeza mahitaji ya nchini.

Takwimu hizo za wizara zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwisho wa mwaka 2024, mtandao wa barabara za vijijini wa China ulikuwa umefikia urefu wa kilomita milioni 4.64.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha