Tanzania yatafuta kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Mkoa wa Shaanxi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 29, 2025

Quan Jian (kushoto), mkuu wa ujumbe wa uchumi na biashara wa Mkoa wa Shaanxi, China na Joseph Simbakalia, mjumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Kuhimiza Urafiki kati ya Tanzania na China, wakiwa kwenye picha jijini Dar es Salaam, Tanzania, Oktoba 27, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM - Tanzania imethibitisha tena dhamira yake ya kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China kwenye Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Kibiashara kati ya China (Shaanxi) na Tanzania uliofanyika Jumatatu wiki hii mjini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Mkutano huo ulioandaliwa kwa ushirikiano na Baraza dogo la Shaanxi la Baraza la Kuhimiza Biashara ya Kimataifa la China (CCPIT) na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), uliwaleta pamoja maafisa wa serikali, viongozi wa biashara, na wawekezaji kutoka pande zote mbili ili kuendeleza maeneo mapya ya ushirikiano katika biashara, viwanda, kilimo, na mageuzi ya kidijitali.

Joseph Simbakalia, mjumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Kuhimiza Urafiki kati ya Tanzania na China, amepongeza mkutano huo akiuelezea kuwa ni mwendelezo wa urafiki wa kudumu kati ya Tanzania na China.

Wajumbe wa ujumbe wa kiuchumi na kibiashara wa Mkoa wa Shaanxi, China wakifanya mazungumzo na maafisa husika kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) jijini Dar es Salaam, Tanzania, Oktoba 27, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

"Mustakabali wa ushirikiano kati ya Tanzania na China upo katika kuugeuza urafiki huu kuwa miradi halisi inayotengeneza utajiri, ajira, na ustawi wa pamoja kwa watu wetu," amesema.

Daudi Riganda, meneja wa kuhimiza uwekezaji wa kigeni wa TISEZA, amethibitisha tena utayari wa Tanzania kuvutia wawekezaji zaidi wa China, hasa kutoka Mkoa wa Shaanxi, chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 na Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Miaka Mitano wa nchi hiyo, ambao unasisitiza ujenzi wa viwanda, maendeleo ya miundombinu, na mageuzi ya kidijitali.

Quan Jian, mkuu wa ujumbe wa kiuchumi na kibiashara wa mkoa huo wa Shaanxi, amezungumzia faida bora za kimkakati za Mkoa wa Shaanxi, zikiwemo rasilimali nyingi za nishati, uwezo mkubwa wa kiviwanda na teknolojia, na msingi ulioendelezwa vizuri wa elimu na utafiti.

Ametaja maeneo matatu muhimu ya ushirikiano wa siku za baadaye, yakiwemo ya nyanja ya kijani, kilimo na nyanja ya mafungamano ya uchumi wa kidijitali, na mawasiliano ya kitamaduni na kielimu.

"Kampuni za Shaanxi zinapenda kushirikiana na Tanzania ili kuendeleza miradi ya nishati ya kijani, kuhimiza kilimo cha kidijitali, na kupanua mikondo ya biashara ya mtandaoni ambayo inaunganisha bidhaa za Tanzania kama vile parachichi na ufuta na soko la China," Quan amesema.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha