Msemaji: Rais Xi Jinping kukutana na Rais Trump leo Alhamisi Oktoba 30 nchini Korea Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 30, 2025

BEIJING - Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilitangaza jana Jumatano ikisema, China na Marekani zimekubaliana kwa kauli moja kwamba Rais Xi Jinping atakutana na Rais Donald Trump huko Busan, Jamhuri ya Korea (ROK), leo Alhamisi Oktoba 30 kwa saa za Korea ili kubadilishana maoni juu ya uhusiano wa pande mbili na masuala yanayofuatiliwa na pande zote mbili.

Msemaji wa wizara hiyo Guo Jiakun amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba shughuli ya diplomasia ya wakuu wa nchi inafanya kazi ya uelekezaji wa kimkakati usio na mbadala katika uhusiano kati ya China na Marekani.

Guo amesema, kwenye mkutano huo nchini Korea Kusini, wakuu hao wawili wa nchi watabadilishana mawazo kwa kina juu ya masuala ya kimkakati na ya muda mrefu kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani, pamoja na masuala makubwa yanayofuatiliwa kwa pamoja.

"Tunapenda kufanya juhudi za pamoja na upande wa Marekani ili mkutano huo kupata matokeo ya kuhimiza hamasa, ambayo yataweza kutoa dira na msukumo mpya kwa ajili ya maendeleo tulivu ya uhusiano wa pande mbili," Guo amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha