Trela: Guangzhou kupitia macho ya msafiri Mhispania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 31, 2025

Mvuto uliofichwa wa Guangzhou — Mji Mkuu wa Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China — unakwenda mbali zaidi ya Mnara wake maarufu wa Canton. Unapatikana katika ladha chungutamu ya inayobaki baada ya kunywa ya chai ya mitishamba, mila na desturi ya kusuuza bakuli na vijiti vya kulia chakula (chopsticks) kwa maji ya moto kabla ya mlo, mchanganyiko endelevu wa mambo ya jadi na usasa, na hata katika msisimko usiotarajiwa wa kukutana na bingwa wa Olimpiki katika kona ya mtaani.

People's Daily Online punde itatoa "Simulizi za Miji | Guangzhou," kipindi kipya kabisa katika mfululizo wake wa video. Jiunge na msafiri Mhispania Alvaro Lago anapogundua mapigo motomoto ya Guangzhou wakati mji huo ukijiandaa kuwa mwenyeji wa ufunguzi wa Michezo ya 15 ya Kitaifa ya China Novemba 9, 2025.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha