Rais wa Tanzania Zanzibar Hussein Ali Mwinyi ashinda uchaguzi wa rais kwa muhula mwingine mpya

(CRI Online) Oktoba 31, 2025

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) jana Alhamisi usiku imemtangaza Rais wa Tanzania Zanzibar Dr. Hussein Ali Mwinyi kuwa mshindi wa nafasi hiyo kwa muhula wa pili.

Mwenyekiti wa ZEC Bw. George Joseph Kazi amesema, Dr. Mwinyi, mgombea wa chama tawala cha CCM, ameshinda kwa uchaguzi huo kwa kupata asilimia 74.8 ya kura zote halali zilizopigwa katika uchaguzi uliofanyika Jumatano wiki hii, akiwashinda wagombea 10 kutoka vyama vya upinzani.

Katika hotuba yake ya kukubali matokeo hayo iliyorushwa moja kwa moja na vyombo vya habari, Dr. Mwinyi ameahidi kuweka maslahi ya taifa mbele katika utawala wake wa muhula mpya, na kuwaomba wagombea wenzake 10 wa urais wa upinzani kufanya kazi kwa karibu katika kulinda maslahi ya taifa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha