Lugha Nyingine
Watu tisa wafariki kwenye maporomoko ya matope huko Kween na Bukwo nchini Uganda
(CRI Online) Oktoba 31, 2025
Maporomoko makubwa ya matope yaliyosababishwa na mvua kubwa usiku wa Jumatano yamevikumba vijiji vya wilaya za Kween na Bukwo nchini Uganda, na kusababisha vifo vya watu tisa, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa, na mamia ya familia kupoteza makazi yao.
Kwa mujibu wa wakaazi wa huko, maporomoko hayo yalitokea wakati kukiwa na mafuriko katika baadhi ya maeneo, yaliyosababishwa na mvua kubwa ya usiku kucha ambayo imezifanya sehemu za barabara kuu kufunikwa au kuzungukwa na maji.
Uharibifu huo umewaacha wanakijiji katika mshtuko, huku ekari nyingi za mazao zikiwa zimezama na nyumba kadhaa zikiwa zimebomoka.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



