China ina nia ya kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na Kuwait, asema Makamu Rais wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 03, 2025

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Emir wa Kuwait Sheikh Mishal Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah huko Kuwait City, Kuwait, Novemba 2, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Emir wa Kuwait Sheikh Mishal Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah huko Kuwait City, Kuwait, Novemba 2, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)

KUWAIT CITY - China inaweka umuhimu mkubwa kwenye uhusiano kati ya China na Kuwait na ina nia ya kuhimiza ushirikiano wa kivitendo wa pande mbili katika nyanja mbalimbali, amesema Makamu Rais wa China Han Zheng wakati wa ziara yake katika nchi hiyo ya Ghuba kuanzia Jumamosi hadi Jumapili ambapo alikutana kwa nyakati tofauti na Emir wa Kuwait Sheikh Mishal Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah, Mwanamfalme Sheikh Sabah Al-Khaled Al-Sabah, na Waziri Mkuu Sheikh Ahmad Al-Abdullah Al-Sabah.

Wakati akikutana na emir wa Kuwait, Han alifikisha salamu za dhati na za kutakia kila la kheri kutoka kwa Rais Xi Jinping wa China.

Han amesema kwamba China daima inathamini urafiki wake na Kuwait na inaweka umuhimu mkubwa katika kuendeleza uhusiano wao.

"Tangu 2022, Rais Xi na Emir wa Kuwait wameshakutana mara mbili na kufikia makubaliano mbalimbali muhimu, wakitoa mwongozo wa kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Kuwait katika ngazi za juu zaidi," Han ameongeza.

Amesema kwamba mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umetuma ishara dhahiri kwamba China inasukuma zaidi mageuzi kwa pande zote na kupanua ufunguaji mlango wa ngazi ya juu, ambayo itatoa fursa kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Kuwait.

Amesema China ina nia ya kushirikiana na Kuwait ili kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa, kutekeleza nyaraka za ushirikiano wa pande mbili zilizosainiwa mbele ya wakuu hao wawili wa nchi, na kujitahidi kwa upigaji hatua mkubwa katika siku za mapema, ili kufikia maendeleo ya kina na imara ya ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Kuwait.

Emir wa Kuwait, kwa upande wake, amemwomba Han kumfikishia heshima yake ya juu kwa Rais Xi.

Emir amesema kuwa Kuwait ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu katika Eneo la Ghuba kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China, ambayo inaonyesha uhusiano wa pande mbili wenye hali ya kimkakati na ya kutazama siku za baadaye.

Akisisitiza tena Kuwait inashikilia bila kuyumbayumba sera ya kuwepo kwa China moja, ameeleza nia ya Kuwait ya kushirikiana na China ili kujenga kwa pamoja Ukanda Mmoja, Njia Moja, kutekeleza ipasavyo nyaraka husika za ushirikiano wa pande mbili, na kusukuma uhusiano kati ya Kuwait na China katika ngazi za juu zaidi.

Wakati akifanya mazungumzo na Mwanamfalme wa Kuwait, Han amesema kwamba Kuwait ni nchi yenye ushawishi wa kipekee na muhimu katika Mashariki ya Kati, na China siku zote imekuwa ikiiweka Kuwait katika nafasi muhimu kwenye sera yake ya mambo ya nje katika eneo hilo.

Wakati akikutana na waziri mkuu wa Kuwait, Han amesema China na Kuwait ni marafiki na washirika wazuri, na uhusiano wa pande mbili katika miaka ya hivi karibuni umepata maendeleo mazuri.

Wakati wa ziara yake nchini humo, Han alishiriki kwenye hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Mwanamfalme huyo wa Kuwait.

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Mwanamfalme wa Kuwait Sheikh Sabah Al-Khaled Al-Sabah, Kuwait City, Kuwait, Novemba 2, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Mwanamfalme wa Kuwait Sheikh Sabah Al-Khaled Al-Sabah, Kuwait City, Kuwait, Novemba 2, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Waziri Mkuu wa Kuwait Sheikh Ahmad Abdullah Al-Ahmad Al-Sabah, Kuwait City, Kuwait, Novemba 2, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Waziri Mkuu wa Kuwait Sheikh Ahmad Abdullah Al-Ahmad Al-Sabah, Kuwait City, Kuwait, Novemba 2, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha