Umoja wa Afrika wampongeza Samia Suluhu Hassan kushinda uchaguzi mkuu wa Tanzania

(CRI Online) Novemba 03, 2025

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf amempongeza Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Tanzania.

Juzi Jumamosi, Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania ilimtangaza Rais Samia ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa ameshashinda uchaguzi mkuu kwa kupata asilimia 97.66 ya kura zote halali zilizopigwa.

Mwenyekiti Youssouf pia ametoa rambirambi kwa familia za watu waliopoteza maisha yao katika maandamano kabla na baada ya uchaguzi huo. Amewahimiza Watanzania kutumia haki zao kwa njia ya amani na kuwajibika, na kutoa wito kwa mamlaka husika kulinda haki hizo kwa kufuata sheria.

Amesisitiza kuwa Umoja wa Afrika uko tayari kuunga mkono kithabiti juhudi za serikali ya Tanzania na watu wake katika kulinda amani, kuhimiza mshikamano wa taifa na demokrasia.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha